.
WANANCHI
katika Kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Iringa wamepata furaha iliyopindukia na baadae kuikataa
Boti iliyopelekwa na Mbunge wao Deo Filikunjombe kama ‘Ambulance’ kwa ajili ya
wagonjwa baada ya mbunge huyo kuwapelekea tena mganga katika zahanati yao.
Kilio
cha muda mrefu kwa Wananchi wa Kilondo ni mganga ndiyo maana mbunge wao
alipowapelekea mganga na boti kwa wakati mmoja walichagua mganga na kusema
hakuna haja ya boti kwa sababu waliomba boti ili kuwasafirisha wagonjwa
kuwapeleka kwa mganga.
Uamuzi
wa mbunge huyo kuamua kutoa fedha yake ya mfukoni na kuwalipa posho waganga
wastaafu ulikuja baada ya Halmashauri ya Wilaya kushindwa kupeleka waganga
katika zahanati hizo huku wananchi wakipoteza maisha kwa magonjwa ya kawaida.
Akizungumza
katika kikao cha Baraza Kuu la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni Bw.
Filikunjombe alisema kuwa wananchi wa Kilondo ni binadamu kama walivyo wengine,
lakini wanakosa huduma muhimu pengine kutokana na mazingira magumu ya Kata na wilaya nzima .
Alisema
kuwa kuna haja ya kuweka mkakati wa kudumu hasa kwa kuwasomesha vijana wa
kutoka mazingira yale na kuingia nao mkataba shida itakwisha.akaongeza kuwa
kote kuna mazingira magumu, lakini Kilondo kuna mazingira magumu zaidi kuliko
Ibumi.
Mkakati
huu ni vema uanze sasa lakini pia kwa kuwa mmeridhia kuwa wapelekwe waganga
wastaafu kwa muda kutokana na kukosekana kwa waganga niko tayari kuchangia
wakati Halmashauri inafanya mkakati wa kudumu kupata waganga katika zahanati ya
Kilondo na Lifuma. alisema mbunge huyo.
Habari
kutoka ndani ya ofisi ya utumishi zinasema watumishi hao wastaafu ambao ni
Martha Ngalawa (Lifuma) na Philipo Kayombo Mbufu (Kilondo) watalipwa posho
kulingana na mshahara waliokuwa wakipata kabla ya kustaafu kwao.
Mbunge
huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani kushiriana na watendaji wa
Halmashauri kuliko kuwindana kwani kufanya hivyo kutadhoofisha maendeleo ya
wananchi, akahimiza kufanyakazi kama timu kwa upendo kwa sababu lengo ni moja.
Bw
Deo aliwaagiza viongozi, watendaji na bodi ya zabuni kuangalia na kutoa
kipaumbele kwa kuwapa kazi makandarasi wa ndani wazalendo wenye uwezo ili
kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya halmashauri kuliko kutoa tenda zote kwa
wageni ambao baada ya kumaliza huondoka na fedha nje ya wilaya.
Akiwakilisha
hoja kwa niaba ya baraza, Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Masasi Bi Lucy Haule
alisema kuwa madiwani wa Ludewa wanakuwa
wakiimba wimbo mmoja akimaanisha kuwa kutokana na shida inayowakabili wananchi
wa mwambao na kuwa Halmashauri imepata
magari mawili ya wagonjwa ni vema na haki moja liende mwambao.
“Kutokana
na shida iliyopo Kata ya Lupingu hasa inayowakabili wagonjwa na wajawazito
baraza lako tukufu linaaigiza kwamba gari moja la wagonjwa lipelekwe katika
kituo cha Lupingu kupunguza tatizo,” alisisitiza Bi. Lucy.
Baada
ya kutoa agizo madiwani wote kwa kauli moja waungamkono hoja na kumwagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa Bi Hilda Lauo kutekeleza agiza hilo bila
kuchelewa na tayari gari hilo limeshapelekwa Lupingu.
Filikunjombe
aliwashukuru madiwani kwa kuridhia kwa upendo na utayari wa kuruhusu gari la
wagonjwa kwenda kusaidia mwambao wa Ziwa Nyasa badala ya Mlangali, lakini
aliahidi kulisimamia na kulifuatilia gari la Mlangali ili liweze kufika haraka.
No comments:
Post a Comment