Na Gustav Chahe, Tanga.
ILE tabia ya baadhi ya wanachi kupenda kukaa vijiweni kucheza
bao na kunywa kahawa kwa kigezo cha umwinyi imeelezwa kupungua siku hadi
siku hatua ambayo ni ishara njema kwa uchumi wa Tanga na ustawi wa Taifa.
Akifungua hoteli ya NYUMBANI HOTELS and RESORTS
tawi la Tanga iliyopo mtaa wa Uhuru, Waziri wa uchukuzi, mawasiliano
na Mbunge wa Tanga mjini Mhesh. Omari Nundu amewataka wawekezaji kutambua
fursa za uchumi ikiwemo utalii ili kuendeleza jiji hilo.
Waziri Nundu alisema kwa kuboresha vituo hivyo kutaleta pia
ushindani wa utalii nchini na kuongeza fursa za ajira kwa wazawa hususani
vijana ambao wengi wao sasa wamekuwa na muamko wa kujituma, wakulima pamoja
na uboreshaji wa miundombinu.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa hoteli hiyo John Kessy akiongea
na waandishi wa habari hotelini hapo amewataka wananchi kutambua huduma
zitolewazo hotelini hapo pamoja na kuzitumia ili kukuza soko la bidhaa zao
yakiwemo mazao kwa kuzingatia hoteli hiyo itakuwa ikitoa huduma zinazotokana
na mazao yao wenyewe.
Kassy amewaomba wananchi kupeleka mazao yao ya mashambani kwa
ajili ya kujipatia kipato na kwamba hoteli hiyo itakuwa ikizingatia utoaji
wa ajira kwa wazawa ambapo hadi kukamilika wanatarajia kutoa ajira 56.
Hoteli ya jiji la Tanga ni ya tatu ikifuatia kwa ya pili
ambayo ipo Moshi mkoani Kilimanjaro wakati ya kwanza ikiwa jijini Mwanza
ambapo ya Tanga ujenzi wake umegharimu bilioni nne hadi kukamilika ikiwa na
vyumba ishirini na vinane vya kulala wageni, kumbi mbalimbali za mikutano
na sehemu za kuogelea.
|
No comments:
Post a Comment