Na Mwandishi Wetu
Kwa wale ndugu zangu hasa wa kuajiriwa na watu binafsi au na mashirika yasiyo ya serikali kama vile ya kidini na mengineyo hii inaweza kuwa imekutokea au umeishuhudia mwajiriwa mwenzio akitendewa.
Suala la upendeleo makazini si suala geni sana kwa asasi zisizo za kiserikali, upendeleo huu ambao mabosi huwafanyia baadhi ya watu fulani katika kampuni au shirika, kwa matakwa yao, kujipendekeza au kwa vigezo vingine visivyo vya maana. Watu hao wachache hupewa nafasi hizo za upendeleo kuliko wengine.
Nafasi hizo ni katika nyanja mbalimbali mfano, vipaumbele katika elimu na mafunzo mbalimbali, safari zenye posho, ruhusa pindi wana-pohitaji, upendeleo katika mishahara na mengineyo mengi ili kuwafurahisha watu hao makazini.
Kwa kawaida hali hii huwanufaisha sana watu hawa wachache ambao ni pendeleo la mwajiri (nyota ya bosi) kwani, vipaumbele hivyo huwa na manufaa sana kwao, lakini hali hiyo huwa kinyume kwa waajiriwa wengine pindi wanapobaini kuwa kuna ubaguzi wa namna fulani katika maeneo yao ya kazi.
Kuna mifano mingi ya hali za ubaguzi na upendeleo makazini, ila nilipoguswa na kukerwa leo ni upande wa mabosi kupanga mishahara jinsi wanavyojisikia bila kuzingatia majukumu ya wafanyakazi hao na vigezi vingine vya muhimu kama elimu na muda wakutumika katika kampuni kama ilivyo kwa asasi za serikali ambako wao hutumia viwango halali kwa vigezo maalumu(TGS Scale). Utakuta katika Kampuni wafanyakazi wameajiriwa kwa muda mmoja na wanakiwango cha elimu kina-cholingana na wanafanya majukumu ya aina moja cha ajabu na cha kushangaza unakuta wanalipwa mishahara tofauti, hali hii inakera sana.
Kwani mfanyakazi anayelipwa kawaida hatoweza kuwa na moyo wa kazi, na yule anayelipwa zaidi kuliko wengine kujiona bora zaidi, cha kushangaza utakuta majukumu anayoyafanya ni ya kawaida ukilinganisha na majukumu yanayofanywa na wafanyakazi ambao wanalipwa mishahara ya kawaida.
Upendeleo makazini unakera sana, kwani unamfanya mfanyakazi kujiona mnyonge na asiye na thamani, na hali hii inampunguzia mfanyakazi uwezo wa kufikiri mambo ya kuinufaisha kampuni au shirika, kwani mara zote atakuwa anafikiria kwa nini anabaguliwa au kwanini hasikilizwi.
Hali ya upendeleo makazini hupelekea waajiriwa wasiopewa vipaumbele kupunguza ari ya utendaji kazi kwa kuona kuwa kazi zao hazithaminiwi na kuoekana kama wanamchango mdogo katika Kampuni kutokana na matabaka mwajiri anayokuwa ameyatengeneza kwa dhima ya upendeleo katika uongozi na utawala wake.
Hali ya kupungua kwa ushirikiano na mara zote huathiri kampuni kwani wafanyakazi hufanya kazi kwa kusukumwa na si kwa kuipenda tena kutokana na hali hiyo ya kubaguliwa na upendeleo miongoni mwao.
Nini kifanyike sasa, ili kupunguza madhara haya katika sehemu za kazi, waajiri wanatakiwa kuwa na sababu za msingi na za kuridhisha za kutoa nafasi hizo za upendeleo kwa wafanyakazi na pia kila mfanyakazi afanywe sawa na wengine iwapo hasa kama ana vigezo vinavyolingana na kupata upendeleo huo.
Hivyo basi waajiri badilikeni fanyeni yaliyo haki na punguzeni mambo ya upendeleo usiokuwa na sababu zenye mashiko. Ili kazi ifanyike vizuri mnahitajika kufanya mambo yakuwaunganisha wafanyakazi wenu na si kuwajengea matabaka yasiyo ya msingi na kwa vigezo vya kipuuzi.
JUA SHERIA TENDA HAKI!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment