Afisa Mwandamizi wa Shughuli (Senior Operations Officer) wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma Bw. Bernabers W. Ndunguru ametoa wito
Baadhi ya wafanyakazi wa Abasia ya Peramiho wakipitia vipeperushi mbalimbali waktati semina ilioendeshwa na maafisa kutoka Mfuko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma.
Mwakilishi wa mwajiri wa Abasia ya Peramho, Bw. Kelvin Zenda akiwatambulisha maafisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma kwa wanachama ambao ni wafanyakazi wa Abasia ya Peramiho wakati wa semina katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Peramiho. Kutoka kulia kwake ni Bw. Barnabers W. Ndunguru (Senior Operations Officer NSSF Ruvuma), kushoto kwake ni Bw. Mussa Adam (Compliance Officer NSSR Songea) akifuatiwa na Bw. Michael William (Compliance Officer, Songea). (Picha na Friday Simbaya)
Afisa huyo mwandamizi alitoa rai wakati semina kwa wanachama ambao ni wafanyakazi wa Abasia ya Peramiho, Songea mkoani Ruvuma kuhusu huduma mbalimbali zinazotoliwa na mfuko huo, iliofanyika tarehe 05.10.2013 katika Ukumbi wa Trade School.
Alisema kuwa mwajiri anawajibu kisheria kujiandikisha kuwa mwajiri mchangiaji na kuandikisha wafanyakazi kwa kupeleka michango ya wanachama kila mwezi.
Aliongeza kuwa mwajiri atafanya makato ya asilimia 10 ya jumla ya mapato yote ya mfanyakazi wake kwa mwezi na naye kama mwajiri kuchangia asilimia 10, sawa na mapato ya mfanyakazi huyo n na kuwakilisha jumla ya makato hayo 20% kila mwezi kwenye shirika kama mchango wa mfanyakazi.
Kwa upande wake Afisa mafuatiliaji wa mfuko ofisi katika ofisi ya Songea (Compliance Officer), Mussa Adma alielezea mafao mbalimbali ambayo yapo chini ya NSSF kwa wanachama. Bw. Adam alifafanua kuwa kuna aina kuu mbili ya mafao yanayotolea na mfuko, ambayo ni mafao ya muda mrefu na mafao ya muda mfupi.
Alisema kuwa mafao ambayo yako chini ya mafao ya muda mrefu ni mafao ya pensheni ya uzeeni, mafao ya mkupuo maalum, pensheni ya ulemavu na pensheni ya urithi.
Katika mafao ya muda mfupi kuna mafao ya matibabu (SHIB), ambao hutolewa kwa wanachama na wategemezi wake ambao ni mume/mke na watoto wasiozidi wanne wenye umri usiodizi miaka 18 au 21 ikiwa wanasoma mafao ya uzazi, mafao ya kuumia kazini na mafao ya msaada wa mazishi.
No comments:
Post a Comment