Na Friday Simbaya,
Songea
Katibu Mkuu wa Chama cha
Wafanyakazi Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE) Taifa , Edson Eliya Kivelege amewataka waajiri nchini kuwalipa wafanyakazi mapunjo ya mishahara yanayotokana
kupandishwa kwa kima cha chini cha mishahara na serikali mwaka jana
kabla ya sheria haijakuchua mkondo wake.
Alisema mapunjo hayo
yanatokana na waajiri wengi wa makampuni
ya walinzi binafasi kutolipa viwango
vipya vya mishahara baada ya serikali kupitia
bodi ya mishahara kutangaza kima cha chini kwa sekta zote mwezi wa saba mwaka
2013.
Katibu huyo wa TUPSE
alisema hayo wakati wa mahojiano
maalum na NIPASHE alipofanya ziara yake katika Nyanda za Juu Kusini
kwa lengo kukagua uhai wa chama pamoja
na kufanya maandalizi ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa mwaka utakaofanyika
hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Aidha, Kivelege alimteua
Zacharia Godwin Mfilinge kuwa mwakilishi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,
ambayo ni mikoa ya Ruvuma ,
Lindi na Mtwara.
Alisema
kuwa kuna baadhi ya makampuni ya walinzi
binafsi ambao bado hawajaanza kutekeleza agizo la Serikali la kupandisha mishahara ya wanafanyakazi kwa
mfano, asilimia 46.4 kwa sekta binafsi kama
ilivyopendekezwa na bodi ya mishahara nchini.
“Tutaanza
kuwahesabia waajiri mapunjo kwa wafanyakazi kwa wanachama wote wa TUPSE kuanzia
Januari mwaka huu. Serikali kupitia bodi
ya mishahara nchini litangaza viwango mbalimabli vya mishahara ikiwemo sekta
binafsi, ambapo walitakiwa kuanza kulipa viwango hivyo mwisoni mwa mwezi wa
saba mwaka jana, ” alifafanua Kivelege.
Aliongeza kuwa, “Makampuni
madogo ya ulinzi ambayo yana wafanyakazi chini ya 100 watakiwa kulipa wafanyakazi
kima cha chini cha mshahara cha shilingi 105,000/- na makampuni makubwa ambayo
yana wafanyakazi zaidi ya 100, basi walipwe Shilingi Laki Moja na Nusu (150,000/-)
kima cha chini cha mshahara yao !”
Wakati wa ziara yake katibu
huyo wa TUPSE alitembelea pia Ofisi ya Afisa wa Kazi mkoani wa Ruvuma pamoja na baadhi
ya ,vyama vya wafanyakazi vya TUICO,
TIPWU, TULGU na TUGHE vilivyopo mkoani
hapa kwa lengo ya ushirikiano.
Katika hatua nyingine, Kivelege
aliwataka waajiri kuwalipa wafanyakazi mishahara ya kila mwezi kwa wakati ili kupunguza vitendo
vya baadhi ya walinzi kushirki katika wizi malindoni.
“Unapowacheleweshia
mishahara wafanyakazi (walinzi) unawatia katika vishawishi vya kuwa na tamaa ya
kuwaibia matajiri kutokana kuwa na maisha
magumu. Waajiri wanatakiwa kuwalipa wafanyakazi mishahara kila mwezi na kwa
wakati na kama watachelewa basi wawalipe kuanzia
tarehe 5 ya mwezi unaofuata,” alisema.
Alisema
pia kuwa waajiri wanatakiwa kuwalipa
wafanyakazi muda wa ziada (overtime) kama
sheria inavyoelekeza .
“Sheria zipo zinazosimamia saa za kazi kwa sekta binafsi Tanzania . Kipengele kidogo B cha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004
kinaelezea kuhusu saa za kazi. Kiwango cha juu kabisa cha saa za kazi ambacho
mfanyakazi anaruhusiwa na sheria kufanya kazi ni saa 45 kwa juma ambayo ni sawa
na saa tisa (9) kwa siku. Muda wa ziada zaidi ya saa 45 kwa juma lazima ulipwe kama saa za ziada,” alisisitiza katibu huyo.
Wakati
huohuo, Katibu wa TUPSE taifa, Edson Kivelege alisema kuwa wakati wa ziara yake
amebaini kuwepo akaunti nane (8) za benki za matawi ya chama hicho amabazo zilifunguliwa
kinyuma na utaratibu wa TUPSE. Mwisho
No comments:
Post a Comment