Tuesday, 25 February 2014

SHULE YA PERAMIHO GIRLS YAONGOZA KIMKOA MATOKEO KIDATO CHA NNE



Na Friday Simbaya, Songea
Wakati Shule ya St. Francis Girls ya Mbeya ikishika nafasi ya kwanza kitaifa, nayo Shule ya Peramiho Girls ya Ruvuma imeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa pia katika matokeo ya kidato cha nne 2013, imefahamika.
Katika uchunguzi waliofanya na MWANDISHI WA MWENGE, ulimebaini kuwa Shule ya Wasichana Peramiho ya wilayani Songea vijijini, mkoani Ruvuma imeshika nafasi ya kwanza kimkoa kati jumla ya shule 113 na kushika nafasi 21 kitaifa kati jumla ya 3256 nchini.
Akizungumza na Mkuu wa Shule, Bi. Lucida Msabila alisema kwamba alikuwa na uhakika wa shule yake kufanya vizuri kutoka na maandalizi mazuri waliopata wanafunzi wa shule hiyo katika masomo.
Akielezea siri ya mafankio hayo Msabila alisema shule yake ilifanya vizuri kutokana ushirikiano mzuri ulipo kati ya wanafunzi, walimu na wazazi, ambapo mwaka 2012 lifanikiwa  kushika nafasi ya pili kimkoa.
“Siri ya mafanikio nikujipanga tu kutoka mwanzo pamoja na kuwa na mpango kazi kwa kuhakikisha Walimu wanafundishia masomo na kama Mwalimu hakumalizi masomo ni lazima afundishe muda wa wikiendi ili kufidia vipindi walivyoruka..” alisema Msabila.
Alisema kuwa mwaka jana shule hiyo ilishika nafasi ya pili kimkoa lakini kitaifa matokeo ya kidato cha nne yalikuwa mabovu, na kuongeza kuwa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka huu hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri na daraja nne lakini kuna mwanafunzi moja tu aliyepata daraja la tatu.
Shule ya Wasichana ya Peramiho pamoja na mafankio pia zipo changamoto kama vile upungufu wa vitabu vya uraia, historia, jeografia na fizikia pamoja na utitiri wa vitabu ambayo unawapashida kipi kutumike.
“Changamoto nyingine ni wanafunzi wengi hawapo tayari kusomo kwa hivyo kama uongozi wa shule tunalazimika kuwasimamia kwa ukaribu…” alielezea Msabila.
Shule hiyo ya Peramiho girls ambayo inamilikiwa na masista wa Mtakatifu Scholastica (Missionary Benedictine Sisters of Tutzing) ilianza mwaka 1968, na Lucida Msabila ni mwalimu mkuu wa 13 tangu 2004 mpaka sasa.
Hata hivyo mkuu huyo
aliponda mfumo mpya wa upangaji matokeo kuwa hautaonesha uhalisia ya mwanafunzi kufanya vizuri ukizingatia kwamba tupo katika jumuiya ya Afrika mashariki na hawata himili ushindani wa soko la ajira la kimataifa hapo baadae.
Shule hiyo imetoa viongozi wengi wa kitaifa wakiwemo spika wa bunge wa sasa Anna Makinda na naibu Waziri wa elimu wa sasa Jenister Mhagama.
Hivi karibuni Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), lilitangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne 2013, huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 15.17. Matokeo hayo ni ya kwanza kutumika kwa mfumo mpya ambao umepanua wigo wa alama na madaraja, hivyo kutoa nafasi zaidi kwa watahiniwa kufaulu.
Akitangaza matokeo hayo jijini Da er Salaam Kaimu Katibu Mtendaji, Dk. Charles Msonde alisema waliofaulu mtihani ni 235,227 sawa na asilimia 58.25 ya 404,083 ya waliofanya mtihani huo, ukilinganisha na 185,940 mwaka 2012, sawa na asiliamia 43.08.
Dk. Msonde alisema matokea haya yalipangwa kwa kutumia alama zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome mwaka jana.
Alama hizo ni A: 75-100, B+: 60-74, B: 50-59, C: 40-49, D: 30-39, E: 20-29 na F: 0-19. Kabla ya mabadiliko hayo, alama zilizokuwa zinatumika kupanga matokeo ya kidato cha nne ni A: 80-100, B: 65-79, C: 50-64, D: 35-49 na F: 0-34.
Dk. Msonde alisema wasichana waliofaulu ni 90,064 sawa na asilimia 55.49 na wavulana ni 111,088 sawa na asilimia 58.45.
Mwisho


Mkuu wa Shule Sekondari ya Wasichana Peramiho Lucida Msabila.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...