Na Friday
Simbaya, Songea
Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Mlimani katika Kijiji cha Peramiho ‘B’ wilayani Songea, mkoani
Ruvuma, Bonventura Mhagama kwa kushirikiana na katibu wake, Asante Mbawa amesema mwananchi atakeyetukana matusi hadharani atatozwa faini
ya shilingi elfu hamsini.
Alisema kuwa
kumezuka tabia kwa baadhi ya watu kitongojini kwa makusudi wameamua kutoa
matusi ya nguoni hadharani kwa kisingizio cha kulewa pombe.
Mwenyekiti huyo
alisema hayo jana wakati wa mkutano wa kitongoji, ambapo alisisitiza kwamba ni
wakati wa kutumia sheria ndogondogo kukomesha tabia ya watu kutukana matusi
baada ya kutofautiana kauli.
“Ni lazima
tuishi katika jamii inayozingatia maadili, mtu mzima unapoporomosha matusi
hadharani unamfundisha ni nini mtoto?”
alihoji mwenyekiti huyo.
Alisema kitendo
hicho katika kitongoji hakitavumilika kwa sasa kwa sababu sheria ndogondogo
zitatumika kumshitaki mtu yeyote atakayetukana mwenzake ili mradi kuwepo na
ushahidi.
Katika mambo
mengine mwenyekiti wa kitongoji alitoa rai kwa wananchi wa kitongoji hicho wawe makini na
wageni wanaofika katika maeneo kwa kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa
katika kitongoji na kijiji kizima.
Kauli hiyo
imetolewa baada yakuwepo tabia ya baadhi ya wananchi kufikiwa na wageni bila
kutoa taarifa kwa balozi wa nyumba kumi au kwa mwenyekiti wa kitongoji.
Alisema kuwa ili
kuhakikishakitongoji kinakuwepo na ulinzi na usalama lazima wageni wanapofika
kitongojini kuwe na utaratibu wa kuwaandikisha wageni wa muda kwenye kitabu cha
wageni cha kitongoji.
“Mgeni anafaida
na hasara, mgeni mwingine anakuwa na nia njema na mwingine anaweza kuwa mhalifu
kwa kuja kuchunguza mazingira ya kuiba kwa shirikiana na wenyeji,”alisema
mwenyekiti.
Alisema kuwa
kitabu cha wageni wanaofika kwa muda kipo kitongojini ni lazima wananchi watoe
taarifa ya wageni wao ili kujua wageni wa ngapi wanaingia na kutoka.
Alisisitiza
kuwa mtu yeyote anapofikiwa na mgeni ni lazima atoa taarifa kwa uongozi husika
kwa kumsainisha kitabu cha wageni wa muda ilikujua mgeni amekuja kwa lengo
gani.
“Kuna mambo
mawili hapa unaweza kumpokea mgeni kisirisiri anaweza kuwa ni mgeni wa hasara
au anaweza kufa ghafla nyumbani kwako utafanyaje? Kumbe ungelitoa taarifa inakuwa
rahisi kwako,” alitoa angalizo.
Kwa upande wa
mazingira, aliwaasa wananchi kuwa na tabia yakufanya usafi katika mazingira yao,
kujenga vyoo bora, kuchimba shimo la taka pamoja na kuaacha tabia yakujisaidia
porini kuepuka magonjwa ya mlipuko kama
vile kipindupindu.
“Sisi tupo
mlimani na wenzetu wapo bondeni, tunapojisaidia porini uchafu wote unateremka
chini na kuchafua maji ya kunywa kwenye visima vya wenzetu kwa hiyo lazima
tujenge vyoo bora na bafu ili kupunguza uchafuzi wa mazingira,” alisema Mhagama.
Aidha, Kitongoji
cha Mlimani ni mmoja vitongoji saba vilivyopo katika Kijiji cha Peramiho ‘B’
katika Kata ya Peramiho, vitongoji vingine ni pamoja na Lipinyapinya,
Namatanda, Mchangani, Madukani, Sekondari na Lihangano.
Kitongoji hicho
kina wakazi zaidi 320 kwa taarifa iliyotolewa mkutanoni na Mwenyekiti wa
Kitongoji, Bonventura Mhagama.
Katika hali
isiyo ya kawaida mjumbe mmoja Sidomino Kita Gama alimaarufu Sido,’ pia balozi
wa nyumba kumi (ten cell leader) ambaye
alinyosha mkono wakati wa mkutano
kutaka kujua kwa nini taarifa ya mapato
na matumizi ya kitongoji hicho hayajasomwa kwa miaka minne?
Kwa upande wake
mwenyekiti huyo alikiri kutoitisha mikutano pamoja na kutowasomea wananchi
mapato na matumizi kwa muda mrefu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake
na kuahidi kuitisha mkutano mwingine wakuwasomea mapato na matumizi mwezi wanne
(Aprili 2014).
Mwenyekiti huyo pamoja na mambo mengine aliwaomba radhi wajumbe wa mkutano kwa kupiga magoti mbele mkutano na wajumbe wakamsamehe.
Mwenyekiti huyo pamoja na mambo mengine aliwaomba radhi wajumbe wa mkutano kwa kupiga magoti mbele mkutano na wajumbe wakamsamehe.
“Sababu
mojawapo iliyosababisha kutoitisha mikutano ni pamoja shughuli za kilimo na
wananchi wengi kutofika mikutanoni pindi inapoitishwa na wakati mwingine
mkutano wanapoitishwa kamati mbalimbali huwazinakosekana kwa ajili ya kutoa
taarifa husika,” alifafanua mwenyekiti.
“Kutokana na
sababu ya wananchi wengi kutofika mkutanoni au kuchalewa kufika katika mikutano,
tutajiwekea kanuni ya kuwatoza faini wajumbe wanaoshindwa kufika mkutanoni bila
taarifa au kwa kuchelewa kufika mkutanoni kwa muda uliopangwa, watalipa faini kati
ya shilingi mia tano na elfu moja,”aliongeza.
Wakati huohuo,
Kitongoji cha Mlimani kimeunda mabaraza mawili ya wazee na vijana pamoja na kuunda
vikundi mbalimbali ya vijana ili kuwaunganisha katika taasisi ya mikopo kuwawezesha
kuendesha biashara na kilimo na hatimaye
kuwa kwamua katika lindi ya umasikini.
Katika baraza
huru la wazee walichaguliwa viongozi wakuliongoza baraza hilo, ambapo Nestory Mbena
alichaguliwa kuwa mwenyekiti, Ester Haule alichaguliwa kushika nafasi ya katibu
na mhasibu alichaguliwa Ponsiano Gama.
Kwa upande wa
baraza la vijana, Sofia Ngonyani alichaguliwa kuwa mwenyekiti na katibu wake alikuwa ni Malta Ndunguru.
“Serikali
haiwezi kusaidia mtu mmojammoja, lakini tunapojiunga katika vikundi mbalimbali
na kuvisajili, kutengeza katiba na kufungua akaunti benki ni rahisi serikali
kutusaidia kwa kupitishia pesa kwenye akaunti hizo,” alielezea mwenyekiti.
Mwisho
No comments:
Post a Comment