Katibu wa
Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga akipokea kadi ya
CHADEMA kutoka kwa Desius Nyoni (kushoto) aliyekuwa Afisa Habari
Msaidizi Wilaya ya Mufindi katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika
katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya wa Mufindi, Komredi Miraji Mtaturu akitoa hotuba.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga akihutubia
Wafuasi
na wanachama wa CCM wakishangilwa ushindi wa chama hicho baada kuzoa
wanachama 170 kutoka Chadema katika mkutano wa hadhara wa CCM
uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana. (PICHA NA
FRIDAY SIMBAYA
Alikuwa
ni afisa habari wa CHADEMA Wilaya ya Mufindi, Rubeni Mwagala, akimwaga
manyanga katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kijiji cha
Nyololo, mkoani Iringa jana.
NA FRIDAY SIMBAYA, MUFINDI
CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi kimeisambaratisha ngome ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kufanikiwa kuvuna viongozi na
wanachama 170 wa CHADEMA akiwamo Afisa Habari wa Wilaya hiyo, Rubeni
Mwagala.
Viongozi
na wanachama hao wa CHADEMA wakiongozwa na Rubeni Mwagala, ambaye
alikuwa ni afisa habari wa CHADEMA Wilaya ya Mufindi, walitangaza rasmi
kuachana na chama hicho katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika
katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.
Katibu wa
CCM wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alizindua shina la wakeleketwa CCM
Nyololo na baadaye aliwakabidhi kadi za uanachama wa wanachama wapya
katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa kijiji
hicho.
Viongozi
wengine wa Chadema waliohamia CCM ni pamoja na afisa habari msaidizi wa
wilaya ya mufindi, Desius Nyoni na Afisa habari muamasishaji wa wilaya
hiyo Meja Mfilinge.
Wana
CHADEMA hao waliohamia CCM walikiponda vikali chama hicho kimejaa ubabe,
ukabila na kwa kufanya siasa za vurugu hapa nchini.
Kwa
upande wake afisa habari huyo wa CHADEMA, Rubeni Mwagala aliwaomba radhi
wananchi wa Nyololo kwa polisi kuwapiga mabomu tarehe 2 Septemba mwaka
2012 na kupelekea kuuawa kwa aliyekuwa mwandishi wa kituo cha
televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi katika Kijiji cha Nyololo
wilayani Mufindi, mkoa wa Iringa.
Alisema
kuwa akiwa kama afisa habari wa Chadema wilaya ya Mufindi ndiye
aliyeratibu kufanyika mkutano na kupelekea mwandishi wa habari wa Chanel
Ten Mkoa wa Iringa na Mwenyekiti chama cha waandishi wa habari mkoa wa
Iringa (IPC), Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za polisi na wafuasi
wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Naye
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliwasihi wananchi waKijiji
cha Nyololo na kwengineko wasibeze hatua ya maendeleo yaliyofanywa na
chama tawala.
Alitoa
mifano hiyo ya maendeleo katibu huyo alisema wakati nchi hii inapata
uhuru kutoka kwa wakoloni nchi ilikuwa barabara za lami kilometa 300,
lakini mpaka sasa kuna barabara za lami zenye urefu kilometa 17,800.
Alisema
nchi wakati huo ilikuwa na vyuo vikuu vichache lakini leo hii ina jumla
ya vyuo vikuu 34 na kuongeza kuwa hapo zamani kulikuwa na madakatari
bingwa wachache lakini leo hii kuna madaktari bingwa 5200.
Aliwaasa
pia wananchi kulinda amani iliyopo nchini kama mboni ya jicho na
kuongeza kuwa ni heri kula dagaa kwenye nyumba yenye amani kuliko kula
minofu ya sangara kwenye nyumba ya vita.
Kwa
upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi komradi Miraji Mtaturu
alisema wakati umefika sasa wananchi wa Mufindi kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015, pigeni kura za
hasira baina ya CHADEMA na kisha kuisambaratisha kabisa ngome hiyo
kuwachagua viongozi wa kwa maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment