Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Biashara kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw.
Abdulla Makame Akiwaeleza waandishi wa Habari(hawapo pichani) Kuhusu Mkutano wa
29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Septemba 20 mwaka
huu Jijini Arusha. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara
hiyo Anthony Ishengoma.Picha na Hassan Silayo
Mkutano wa 29 wa Baraza
la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
utapokea na kuidhinisha aina mpya ya hati za kusafiria za kielektroniki,
zikiwemo sampuli za hati za kusafiria za kibalozi, za Maofisa na za
kawaida.
Hayo yamesemwa leo
Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Biashara,Uwekezaji na
shughuli za uzalishaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Abdulla
Makame wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Mkutano huo
utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu Jijini Arusha pia unatarajia kupokea na
kuidhinisha taarifa mbalimbali sambamba na kutolea maamuzi masuala yanayohusu
mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akieleza zaidi Makame
amesema mkutano huo utapokea na kuidhinisha aina mpya ya hati ya kusafiria ya
kielektroniki,zikiwemo sampuli za hati za kusafiria za kibalozi, za
Maofisa na za kawaida za kusafiria.
Aidha Mkutano huo
utajadili mapendekezo na hadidu za rejea za uanzishwaji wa Dira ya maendeleo ya
Afrika Mashariki ya mwaka 2050.
Pia mkutano huo
utajadili mapendekezo ya mpango mwelekeo na shughuli mbalimbali zinazolenga
kuandaa katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki na kujadili mapendekezo ya
baraza la ulinzi na usalama linalopendekezwa.
Baraza la Mawaziri
katika Jumuiya ya Afrika mashariki ni chombo cha pili katika ngazi za kufanya
maamuzi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Mkutano wa Kilele.
No comments:
Post a Comment