Mwenyekti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Iringa Mjini,
Frank Nyalusi akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya kitanzini
leo.
Mkazi wa
Kitanzani Claud Mahembe akiuliza swali la kutaka kupata ufafanuzi kweni
bunge la katiba maalum halisitishwi kwa mwenyekiti wa Chadema Wilaya
Iringa Frank Nyalusi wakati wa mkutano wa hadhara jioni leo.
Na Friday Simbaya, Iringa
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Iringa Mjini limeshindwa
kufanya maandamano ya amani kama ilivyotangazwa kwa kile kilichoelezwa
na Mwenyekiti wake, Frank Nyalusi "tumepokea zuio kali kutoka jeshi la
Polisi."
Akizungumza
katika mkutano wadhara uliyofanyika Kata ya Kitanzaini mjinin Iringa,
Nyalusi alisema wata fanya maandamano hayo Jumatatu wiki ijayo ikiwa ni
kuitikia wito uliotangazwa na Mwenyekiti wao wa Taifa, Freeman Mbowe wa
kufanya maandamano ya amani yasio na ukomo yenye lengo la kushinikiza
kusitishwa kwa Bunge la Katiba.
Alisema
pamoja na jeshi hilo kuwazuia kufanya maandamano jana hiyo hiyo
waliruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wenye machinga
wengi maarufu kama magari mabovu, Kitanzini.
Akieleza
kushangazwa na maamuzi ya Polisi ya kuzuia maandamano yao, Nyalusi
alisema maazimio yaliofikiwa katika mkutano huo nikufanya maandamano
Jumatatu hata bila ya kibali cha polisi.
Wakati
Chadema wakidai kudhibitiwa kufanya maandamano hayo, Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema jeshi hilo halijapokea barua
yoyote kutoka katika chama hicho inayoonesha wameomba kufanya maandamano
hayo.
Akitoa
ufafanuzi huo kwa njia ya simu, Mungi alisema "nchi hii kama zilivyo
nchi nyingine inaendeshwa kwa sheria, taratibu na kanuni."
Alisema
watanzania bila kujali wanatoka kundi gani ni lazima wafanye mambo
wanayotaka kufanya kwa kuzingatia sheria vinginevyo mkono wa sheria
utawafukuzia.
Alisema
mji wa Iringa upo shwari na kwamba jeshi la Polisi limejipanga
kikamilifu kukabiliana na hali yoyote ile itakayoonekana inataka
kuhatarisha amani.
Aliwataka
wakazi wa Iringa kuendelea na shughuli zao kama kawaida na pale
watakahisi au kusikia kuna mtu au kikundi chochote cha watu kinataka
kufanya jambo linaloweza kuhatarisha usalama wao na wa mali zao, watoe
ushirikiano kwa kutoa taarifa Polisi.
No comments:
Post a Comment