Na Mathias Canal, Kwanza Jamii
Mbunge wa
Iringa Mjini Mch Peter Simon Msigwa ametoa mifuko 100 ya Saruji
kumalizia shule ya Sekondari Nduli ili kupunguza usumbufu mkubwa
wanaoupata wananchi wa Kata hiyo kwani wanafunzi wamekuwa wakiteseka
kusoma mbali na kijiji hicho.
Amesema
kuwa tofauti za kisiasa kati yake na Diwani wa Kata hiyo zimemalizika
badala yake ni muda wa kufanya shughuli za maendeleo.
Ameongeza kuwa waliosababisha kuchelewa kufika kwa fedha za mfuko ni wananchi wenyewe hivyo sio sehemu ya yeye kulaumiwa.
Akizungumzia
kuhusu mifuko 100 iliyopelekwa kijijini hapo kabla ya leo kutoa mifuko
hiyo, Msigwa amesema kuwa Chama cha Mapinduzi CCM kilitoa mifuko 100 ya
Saruji baada ya kusikia kuwa anataraji kutoa Saruji hivyo wakaamini
kwamba wamemzima kiutendaji kumbe wamewasaidia wananchi na sio kumkomoa
yeye.
Hata
hivyo wakazi wa kijiji hicho waliojitokeza wamesema kuwa hawatambui
kuletwa mifuko 100 na CCM na kuhoji kama kweli imeletwa wafahamishwe
mahali ilipo wasipo onyeshwa itakuwa ni kiini macho.
Msigwa
amefikia uamuzi wa kuwapatia wananchi hao mifuko 100 baada ya kupata
taarifa kwamba wananchi wanatakiwa kuchangia mifuko 15 aliamua kusitisha
zoezi hilo la kuchangishana wananchi badala yake kuamua kutoa ili
kutowakandamiza wapiga kura ambao ni hazina ya mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment