Monday, 29 September 2014

POLISI INAMSHIKILIA MFANYABIASHARA KWA MAUAJI YA MKE WAKE




Na Friday Simbaya, Iringa
Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mfanyabiashara wa Mjimwema wilayani Mufindi kwa tuhuma za mauaji ya mke wake kutokana wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi alisema kuwa polisi wanamshikiria Pascal Lwila (28) mfanyabiashara wa Mjimwema kwa kumuua mke wake, Naomi Sanga (27) kwa kumpiga ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake.
Akizungumza  mbele ya waandishi wa habari leo ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, alisema kuwa tukio hilo mnamo tarehe 28/09 mwaka huu majira ya saa 9 alfajiri katika maeneo ya Mjimwema katika Kata ya Boma, tarafa ya Ifwagi wilayani Mufindi, mkoa wa Iringa.
Mungi alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi na mtuhumiwa anatarajia kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa linamtafuta Amosi Legunji, mkulima kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mke wa ndoa aliyetambulika kwa jina Helena Mhangawi (33), kwa kumchinja shingo pamoja na kumwondoa sehemu zake siri na kutoweka kusikojulikana.
Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa Iringa ofisini kwake, Ramadhani Mungi alisema kuwa tukio hilo limetokea kijiji cha Mafuruto kilichopo katika Kata ya Mlowa, Tarafa ya Idodi Wilaya ya Iringa vijijini mkoa Iringa.
Awali mke wa mtuhumiwa alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Septemba 23 majira ya saa 2 usiku mwaka huu, ambapo mchana wa Septemba 25 mwili wake ulikutwa na majeraha sehemu mbalimbali huko shingo yake ikiwa imechinjwa pamoja na kuondoa sehemu za siri. Chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...