Na Friday Simbaya,
Iringa
Katibu wa Chama cha Walimu
Tanzania (CWT) Wilaya Iringa Manispaa, Fortunatafatuma Njalale amesema mgeni
rasmi katika kilele cha siku ya waalimu duniani kiwilaya atakuwa Naibu Waziri,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi TAMISEMI, Kasimu Majaliwa (MB).
Alisema kuwa sherehe zinatanguliwa
na juma la elimu siku ya walimu duniani Wilaya ya Iringa Manispaa kuanzia
tarehe 29/09/2014 hadi 01/10/2014 ambapo itakuwa ni siku ya kilele kiwilaya
katika Uwanja wa Samora, ili kujiandaa na sherehe hizo zitakazofanyika kitaifa
mkoani Bukoba tarehe 5 mwezi Oktoba mwaka huu.
“Sisi wilaya na mikoa
huwa tunafanya sherehe hizo siku ya walimu duniani kabla ya kilele kitaifa ili
kuwapa na nafasi viongozi mbalimbali wa wilaya na mikoa kushiriki katika sherehe
za kitaifa ukizingatia Bukoba ni mbali sana…,” alifafanua.
Kila tarehe 5 mwezi wa kumi kila mwaka, huwa
ni siku ya Walimu Duniani. Siku hii ya walimu duniani hutafakari walikotoka na
changamoto wanazopata wakiwa kazini.
Aidha, katibu huyo alisema
kuwa katika juma hilo la sherehe za siku ya walimu duniani kiwalaya chama hicho
kitafanya shughuli mbalimbali pamoja na kuwa na mkutano wa uzinduzi wa ndani,
ambapo mgeni rasmi alitarajia kuwa rais wa CWT Taifa, Gratian Mkoba lakini mgeni
rasmi huyo kwa bahati mbaya amepata hudhuru.
Aliongeza kuwa kutokana
na mabadiliko ya ratiba hiyo wamepanga kukutana na kiongozi huyo wa kitaifa
baada ya sherehe hizo kumalizika kwa ajili ya kuongea na walimu Manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa shughuli
zingine zitakazofanyika katika sherehe hizo ni pamoja na kuona watoto wagonjwa
katika hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa, usafi wa soko katika soko kuu
Manispaa ya Iringa, mashindano ya michezo ya riadha, mashindano ya mpira wa
pete na miguu timu za walimu na timu za nje na hatimaye kufanya maandamano
kuanzia Manispaa ya Iringa hadi katika Uwanja wa Samora kwa ajili ya kilele cha sherehe hizo ki wilaya
hapo tarehe 01/10/2014.
Hata hivyo katibu huyo
alitoa wito kwa walimu wote wa Wilaya ya Manispaa ya Iringa kujitokeza kwa
wingi ili waweze kuonyesha vipaji mbalimbali pamoja kuonyesha ubunifu wao
katika masomo mbalimbali.
Kauli mbiu ya
maandhimisho mwaka huu; wekeza katika elimu kwa ajili ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment