Mgeni
rasmi afande kanali John Julius Mbungo (mwenye miwani) ambaye pia ni
mwanasheria mkuu wa jeshi la kujenga taifa akipokea salamu na baadaye
kukagua gwaride kwa, kumuakilisha mkuu wa jeshi la kujenga taifa kwenye
sherehe ya kumaliza mafunzo ya awali ya kuruti wa JKT kundi la miaka 50
ya muungano (kujitolea na mujibu wa sheria awamu ya kwanza 2014) katika
kikosi cha 841 KJ Mafinga, mkoani Iringa.(PICHA NA FRIDAY SIMBAYA
Kijana wa
kikundi cha kombati karate akionesha umahili wakunyanyua ndoo za maji
kwa meno kwenye sherehe ya kumaliza mafunzo ya awali ya kuruti wa JKT
kundi la miaka 50 ya muungano (kujitolea na mujibu wa sheria awamu ya
kwanza 2014) katika kikosi cha 841 KJ Mafinga, mkoani Iringa. (PICHA NA
FRIDAY SIMBAYA
Kikundi
cha sarakasi kikitoa burudani kwenye sherehe ya kumaliza mafunzo ya
awali ya kuruti wa JKT kundi la miaka 50 ya muungano (kujitolea na
mujibu wa sheria awamu ya kwanza 2014) katika kikosi cha
841 KJ Mafinga, mkoani Iringa leo. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA
841 KJ Mafinga, mkoani Iringa leo. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA
Kikundi
cha kwata ya singe kikipata mbele ya mgeni rasmi na kutoa heshima kwa
mwendo wa mchakamchaka kwenye sherehe ya kumaliza mafunzo ya awali ya
kuruti wa JKT kundi la miaka 50 ya muungano (kujitolea na mujibu wa
sheria awamu ya kwanza 2014) katika kikosi cha 841 KJ Mafinga, mkoani
Iringa (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA
Na Friday Simbaya, Mufindi
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ametoa wito kwa vijana wanaohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi ambao ni vijana wa mujibu wa sheria na wa kujitolea kuzingatia kiapo cha utii walichoapa.
Akitoa wito huo kwa niaba mkuu wa jeshi la kujenga taifa, afande mgeni rasmi Kanali John Julius Mbungo, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa alisema kuwa vijana ni lazima wazingatie kiapo cha utii walichoapa mbele ya mgeni rasmi kwa Amiri Jeshi Mkuu wa
Majeshi na Usalama.
Majeshi na Usalama.
Alisema kuwa mafunzo waliopata ni kwa manufaa ya watanzania na sio kwa manufaa yao binafsi na pia wakumbuke kuweka miili yao ikiwa timamu kimazozi wakati wote.
Kanali Mbungo pia aliwaasa wahitimu hao kutojiingiza katika makundi yasiyofaa katika jamii na kutorubuniwa na makundi yanayotaka kuwagawa watanzania.
"Imarisheni mahusiano ya ushirikiano mliyojijengea mkiwa katika mafunzo haya. Mtumie ujuzi mliopata kuwafundisha na kuwaelekeza vijana ambao hawajapatia mafunzo ya JKT," alisema.
Aidha, wahitimu vijana wa mujibu wa sheria na wa kujitolea katika risala yao kwa afande mgeni rasmi walisema kuwa kulikuwepo na changamoto mbalimbali walizokumbana nazo wakati mafunzo kama vile; uhaba wa mavazi, upungufu wa magari katika mafunzo, uhaba wa maji na kucheleweshea posho pamoja na upungufu wa wakufunzi ukilinganisha na idadi ya wanafunzi.
Wahitimu haon waliiomba serikali kuongeza muda wa mafunzo kwa vijana wa mujibu wa sheria kutoka miezi mitatu sasa hadi kufikia miezi sita iliwaweze kuiva vizuri.
Hata hivyo, afande mgeni rasmi aliwaahidi kuwa changamoto zote zilizopo katika ngazi ya Jeshi la kujenga taifa zitashughulikiwa ipasavyo na kuongeza kuwa zingine ambazo zitakuwa juu ya uwezo wao watazipeleka ngazi ya juu.
"Natambua pia changamoto wanazozipata wakufunzi zikiwemo, upungufu wakufunzi ikilinganisha na idadi ya wanafunzi," alisema.
Sherehe ya kumaliza mafunzo ya awali ya kuruti wa JKT kundi la miaka 50 ya Muungano (kujitolea na mujibu wa sheria awamu ya kwanza 2014) katika kikosi cha 841 KJ Mafinga yalifanyika ambapo zaidi ya vijana 3,000 walihitimu mafunzo hayo jana (Ijumaa wiki) hii mjini Mafinga.
Sherehe hizo pia zilipambwa na burudani kutoka kwa vikundi vya vijana kwa kuonesha maonesho mbalimbali kama vile kwaya, kwata ya singe, kombati karati, ukakamavu, sarakasi, shairi na burudani toka brassband ya 841 KJ.
Jeshi la Kujenga Taifa ni moja kati ya taasisi muhimu mbayo ilianzishwa Julai 10, 1963, ikiwa maalumu kwa ajili ya kuwajengea vijana elimu ya kujitegemea, kuthamini utaifa wao, kujenga maadili ya kizalendo na kuheshimiana bila ubaguzi wa aina yoyote pamoja na kuwajengea ari ya kujitolea na namna ya kudumisha na kuimarisha amani na ulinzi wa taifa.
Vijana wengi, na hasa wasomi wa ngazi mbalimbali walikuwa walengwa katika dhana ya kuanzishwa kwa mafunzo ya kijeshi katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Kujenga Taifa nchini. Matokeo yake mazuri yalijidhihirisha katika maeneo mbalimbali ya kazi maofisini na hata katika kazi za mikono.
Nidhamu ya kufuata maadili mema inahitaji muda na uadilifu katika maandalizi ya hatua za awali kabisa kwa rika la vijana, na ndiyo maana mafunzo ya vijana kupitia Jeshi la Kujenga Taifa yalionekana kuwa mhimili mkubwa katika kuliandaa taifa kuwa na viongozi wazuri na waadilifu kwa miaka ijayo, dhamira ambayo inatakiwa iwe endelevu bila kikomo.
Kwa bahati mbaya sana, mafunzo hayo kwa vijana yalisitishwa mwaka 1994, lakini kwa sasa yamerejeshwa tena na vijana wanaomaliza kidato cha sita pamoja na baadhi ya vyuo vya elimu ya juu wanaendelea na mafunzo katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Kujenga Taifa nchini.
No comments:
Post a Comment