Katibu wa TUPSE Taifa, Edson Eliya Kivelege akiongea na waandishi wa habari muda mfupi wa kutangaza viongozi wa kanda ya nyanda za juu kusini cha chama hicho jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA
Na Friday Simbaya, Iringa
Chama cha Wafanyakazi Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE) Kanda za Nyanda
za juu Kusini kimepata viongozi wapya watakao kuwepo madarakani kwa
kipindi cha miaka mitano, imefahamikia.
Akitangaza majina ya viongozi hao waliochaguliwa katika mkutano
uliofanyika jana Katibu wa TUPSE Taifa, Edson Eliya Kivelege
alimtangaza Yareh Mazengo kuwa mwenyekiti wa kanda.
Wajumbe waliochaguliwa kuunda Kamati Kuu ya Utendaji ni Haruna
Chalala na Selemani Mkwawa, wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa
waliochaguliwa ni Lazaro Msangi, Tujia Nyamoga, Paulo Kaoyama na
Aloyce Mwamakula na mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa wanawake
alichaguliwa Mwanne Ramadhani na Oliver Daniel alichaguliwa kuwa
Kaimu Katibu Kanda za Juu Kusini.
Viongozi hao waliochuguliwa waliahidi kuchapa kazi kwa uweledi na kwa
ufanisi pamoja na kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili
wanachama.
Kivelege aliongeza kuwa Iringa ina jumla ya makampuni ya ulinzi
binafsi 36 nyingi zikitoka nje ya mkoa, lakini pamoja na hayo kampuni
zenye ofisi azizidi kumi (10) na kusababisha kukosa mawasiliano.
Alisema kuwa chama kinapotaka kuwasiliana na wanachama wake kinapata
shida ya kuonana na viongozi kwa ajili yakutatua kero za wanachama kwa
sababu ofisi nyingi za waajiri zipo Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam.
Alisema kuwa kampuni nyingi hapa Iringa zinafanyakazi za udalali kwa
sababu hiyo kampuni hizo zinakuwa zinawaajiri walinzi wasiokidhi
vigezo ambao wanakuwa na uweledi mdogo kuhusiana na masuala ya ulinzi.
"Kazi ya ulinzi ni kazi nyeti ambayo inahitaji mawasiliano ya wazi
kati ya mwajiri na mfanyakazi na mfanyakazi na mteja (watu
wanaowalindia mali) na chama cha wafanyakzi," alisema.
Aliongeza kuwa sare zinatakiwa kutolewa bure kwa walinzi na zitolewe
pea mbili kwa ajili ya kubadilisha na sehemu za baridi walinzi
wapatiwe makoti mazito.
Aliongeza kuwa walinzi wasipopatiwa mavazi na viatu kulingana na hali
ya hewa wanalazimika kutafuta mahala salama na kukoka moto na kulala
malindoni. Pia, alisema kuwa kampuni nyingi za walinzi hazitoi
mikataba kwa
wafanyakazi wala vitambulisho kwa walinzi ambapo inakuwa vigumu
kuwatambua walinzi pindi wanapopata matatizo.
Hata hivyo katibu mkuu huyo waliwataka waajiri kuwalipa nyongeza ya
mishahara kuanzia Juni 1, 2013 sawa na asilimia 46.4 ya kima cha chini
cha mshahara, kama ilivyotangazwa na serikali kupitia bodi ya
mishahara mwaka juzi.
Alitoa wito kwa waajiri pia kufuata utaratibu wa ulipaji wa mishahara
sio kila kampuni kuwa na tarehe yake ya kulipa mshahara na kuwataka
waajiri nchini kuwalipa wafanyakazi mapunjo ya mishahara yanayotokana
na kupandishwa kwa kima cha chini cha mishahara kilichotangazwa na
serikali mwaka jana.
Walisema kuwa kumekuwepo na vitisho kutoka waajiri wao wanapogundua
kwamba wamejiunga vyama vya hiari na pamoja na kuanzisha matawi ya
vyama vya wafanyakazi.
Mwisho

No comments:
Post a Comment