Tuesday, 9 September 2014

WANAFUNZI 21,540 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI IRINGA

 Wanafunzi wa shule ya msingi chemchem katika Manispaa ya Iringa wakiwa juu ya paa la choo  wakisafisha  ikiwa ni sehemu ya maandalizi kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2014 mtihani huo utakaofanyika  tarehe 10 na 11/9/2014, ambapo shule za msingi 458 kati ya shule 484 ndizo zenyewanafunzi watakaofanya mtihani wakumaliza elimu ya msingi mkoani Iringa. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

 https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=148551792f099bb1&attid=0.1&disp=inline&realattid=file0&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9BRHotx0LdPyXvG8i9awjW&sadet=1410257157005&sads=8ez09vR2Miii--otw272s0xIDF8
Afisa Elimu Mkoa wa Iringa, Joseph Mnyikambi akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwaka. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

Na Friday Simbaya, Iringa
Jumla ya wanafunzi 21,540 wakiwemo wavulana 9,779 na wasichana 11,761 ndio watakaofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu mkoani Iringa, imefahamika.

Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2014 utafanyika  tarehe 10 na 11/9/2014, ambapo shule za msingi 458 kati ya shule 484 ndizo zenye wanafunzi watakaofanya mtihani wakumaliza elimu ya msingi.
Akiongea na waandishi wa habari leo, Afisa Elimu Mkoa wa Iringa,
Joseph Mnyikambi alisema idadi ya wanafunzi wanaofanya mtihani mwaka 2014 imepungua ukilinganisha na mwaka jana, 2013 ambapo kulikuwa watahiniwa 23,149 (wavulana 10,753 na wasichana 12,396) waliosajiliwa.
Afisa elimu huyo alisema maandalizi yote yamekamilika, kwani vifaa vyote vinavyohusiana na mtihani vimekwisha pelekwa kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Iringa.
"Wito wangu kwa wazazi wote wenye watoto wanaosoma darasa la saba, wahakikishe watoto wao wanakwenda kufanya mtihani," alisema.
Aliongeza kuwa wanafunzi walio darasa la saba wahakikishe wanazingatia maelekezo watakayopewa na wasimamizi.
Mchanganuo kihamashauri ni kama ifuatavyo; Manispaa ya Iringa
waliosajiliwa mwaka huu ni 3,264, Halmashauri ya Iringa, 5,914, Kilolo, 5,142 na Mufindi wanafunzi waliosajiliwa ni 7,220.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...