RAIS wa
Zanzibar na Mweneykiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein
amemteua Mh. Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Kwa
mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi
ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee, Dkt Shein
amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 55(1)
cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Mheshimiwa
Said Hassan anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
Mh. Othman Masoud Othman ambaye Uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa
Vifungu vya 53, 54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na
Kifungu 12(3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.
Kabla ya Uteuzi huo Mheshimiwa Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Uteuzi huo umeanza tarehe 07, October, 2014.IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment