Wednesday, 8 October 2014

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI ALIYEUAWA KISHA KUPORWA PIKIPIKI HATIMAYE AZIKWA!




Na Friday Simbaya, Iringa
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lugalo, Salehe Khamis (18) aliyeuawa tarehe 06/10/2014 kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasiofahamika kisha kupora pikipiki yake ambayo haijafahamika namba za usajili hatimaye amezikwa jana.

Kamera ya THE SCOOP majira ya mchana ilishuhudia ndugu na jamaa wakisubiri mwiili wa marehemu kuswaliwa katika Msikiti wa Mshindo Manispaa ya Iringa na hatimaye kuelekea katika makaburi ya Makanyagio kwa maziko.
Kamanda wa Polisi mkoani Iringa (RPC),Ramadhani Mungi amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana  kuwa Salehe Khamis (18) aliuawa tarehe 06/10/2014 majira ya saa 6:15 usiku katika Kitongoji cha Kikungwe Igumbilo, Kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa.
RPC alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni pamoja na kuwania mali, ambapo hata hivyo, watuhumiwa wanatafutwa na jeshi la polisi.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...