Katibu mkuu wa CCM Bw kinana kushoto akishiriki kuvua samaki Kalenga na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu |
Kinana akitazama bwawa la samaki na kuvua samaki
Chifu wa wahehe wa pili kulia akiwa na wasaidizi wake huku kiti cha kinana kikiwa tupu |
Mkutano wa Kinana Kalenga |
Mwenuyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stivin Mhapa akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM mbele ya katibu mkuu wa CCM Bw Kinana |
Wanahabari wakiongozwa na mhariri wa habari gazeti la Jamboleo Said Mwishehe kushoto kutazama fuvu la chifu Mkwawa baada ya kutembelea makumbusho hayo jana |
Wanahabari waliopo katika msafara wa Kinana wakitazama fuvu la chifu Mkwawa |
Kinana akiwa ameshika bunduki ambayo chifu Mkwawa alikuwa akiitumia |
Chifu wa wahehe mrithi wa Mkwawa Bw Abdu Mkwawa akitoa maelekezo kwa katibu mkuu wa CCM Bw Kinana mbele ya fuvu la Chifu Mkwawa |
Kikundi cha mamalishe ambao walikuwa Chadema waliojiunga na CCM mbele ya kinana |
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Delophina Mtafilalo akimkabidhi kinana kikapu cha asili . |
KATIBU mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa , Abdulrahman Kinana amesifu utendaji kazi wa mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa kuwa amekuwa ni mfano wa kuingwa kutokana na kuendelea kuwa karibu zaidi na wapiga kura wake.
" Kijana Godfrey Mgimwa ni hodari sana kwani ameendelea kufanya kazi kwa kujituma zaidi kama alivyokuwa marehemu babake ......kweli kijana huyo amenifurahisha sana kwani kipindi hiki anachoongoza si cha kwake ni kipindi cha marehemu babake ila yeye ameendelea kujitolea zaidi na kufanya kama alivyokuwa akifanya babake .....hivyo nampongeza sana mbunge wenu huyo Godfrey Mgimwa "
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana
katika kijiji cha Kalenga alisema kuwa mbunge huyo ameiga tabia ya marehemu babake kwa kuendelea kuwatumikia wapiga kura kwa unyenyekevu mwingi na uwajibikaji wa hali ya juu jambo ambalo kwake binafasi na chama ni njema zaidi.
Kwani alisema kuwa amekuwa akifuatilia katika vyombo mbali mbali vya habari toka alipochaguliwa na kuona jinsi ambavyop mbunge Mgimwa anavyoendelea kuwa karibu zaidi na wapiga kura wake kwa kila juma kufika jimboni kuhamasisha na kuchangia maendeleo ya wana kalenga.
Kinana alisema marehemu Dr Wilaim Mgimwa wakati wa uhai wake hakuwa na makuu na mtu ila alikuwa akipenda kumsaidia kila mmoja na wakati wote alikuwa ni kiongozi msikivu na mpre zaidi mfano ambao ameuiga mwanae Godfrey Mgimwa ambae amekuwa na tabia njema ndani ya chama na kwa wapiga kura wake.
Hata hivyo alisema kuwa ndoto ya wana Kalenga ni kuendelea kuona wanapata maisha bora kwa upande wa wakulima kusaidia kuboreshewa kilimo chao kwa kupata pembejeo ambazo ni hitaji lao kazi ambayo Mgimwa anaiweza kwa kushirikiana na serikali ya wilaya na mkoa.
Kuhusu miradi mikubwa ya kimaendeleo inayoendelea katika jimbo hilo Kinana alisema kwa sasa ipo miradi ya umeme kwa maeneo ambayo hayajapata kuwa na umeme na kuwa umeme huo ni wa gharama nafuu na kudai kuwa zote hizo ni jitihada za mbunge huyo.
Pia Kinana alitaka wananchi viongozi wa serikali katika mkoa wa Iringa na wilaya hiyo kusaidia kuboresha maisha ya wananchi hao kwa kusaidiana na mbunge Mgimwa na kuwa CCM isingependa kuona wananchi wanaendelea kuwa nyuma kuteseka na kero mbali mbali zinazowakabili . (MZEE WA MATUKIO DAIMA)
No comments:
Post a Comment