KATIBU wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Nape Nnauye ambana mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amfananisha na mpangaji na kuwa kodi yake ya kuendelea kudumu katika jimbo hilo imekwisha hivyo ajiandae kufungasha vilago ili uchaguzi mkuu 2015 akabidhi jimbo hilo CCM.
Nnauye alitoa kauli hiyo JANA mara baada ya kuwasili katika jimbo la Iringa mjini kwa ajili ya ziara siku 6 mkoani Iringa na katibu mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana.
" Tutakuwa na ziara mkoa wa Iringa kwa muda wa siku 6 na hadi tukimaliza ziara yetu hapa Iringa chama chetu kitakua juu zaidi hivyo nawaombeni fikisheni salamu kwa wapangaji kuwa kodi yao imekwisha na hivyo tunahitaji watuachie jimbo letu na kwa sasa hatuna mpango wa kupangisha tena," alisema Nnauye huku akishangiliwa na umati wa wananchi wa jimbo la Iringa mjini waliokuwepo katika mapokezi hayo.
Akizungumza na wanachama hao kabla ya kuzindua ofisi ya CCM wilaya ya Iringa vijijini Iliyofanyiwa ukarabati upya katibu mkuu, Abdulrahman Kinana alisema kuwa CCM imeendelea kukamilisha utekelezaji wa ahadi zake ambazo ziliahidiwa mwaka 2010 na kuwa hadi sasa sehemu kubwa ya ahadi hizo imetekelezwa na kilichobaki ni kuwaomba watanzania kuendelea kuwa na imani na CCM ili mwakani 2015 kuendelea kuchagua chama hicho.
Kinana alisema kuwa kazi kubwa imeendelea kufanywa na viongozi wa CCM na serikali yake chini ya Rais Jakaya Kikwete katika kuona watanzania wanaendelea kunufaika na matunda ya serikali yao kwa kusogezewa maendeleo karibu zaidi na kutaja miradi mkubwa ambayo imetekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za lami kila kona ya nchi hii.
" Tunazunguka kuendelea kukijenga zaidi chama lengo ni kuona watanzania wanaendeleo kukiamini chama na kuhamasisha zaidi wananchi kujitokeza kwa wingi katika chaguzi za serikali za mitaa mwaka huu ili kuchagua viongozi wanaotokana na CCM kwani ndicho chama chenye mapenzi ya kweli ya kuliongoza Taifa hivyo hakuna sababu ya watanzania kutokiamini chama cha mapinduzi"
Pia alisema kuwa mbali ya CCM kuendelea kukamilisha utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi bado chama hicho kina mpango mzuri wa watanzania ili kuona mwakani 2015 chama kinashinda na hapa watanzania wategemee ahadi nyingi na kubwa zaidi ya zile za mwaka 2010.
Awali Kinana alimpongeza aliyekuwa mjumbe wa bunge malum la katibu na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kwa jinsi alivyowawakilisha vema wakazi wa mkoa wa Iringa na watanzania kwa ujumla na kuwa alikuwa akimfuatilia na kufurahishwa na uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja.
Kwa upande wake Msambatavangu akimkaribisha katibu mkuu huyo alisema kuwa mbali ya kuwa ziara hiyo inaanzia jimbo la Kalenga kwa upande wa wilaya ya Iringa vijijini ila mbunge wake Bw Godfrey Mgimwa hatafanikiwa kushiriki kutokana na heshima kubwa ambayo spika wa bunge Anne Makinda amempa mbunge huyo kwa kumteua kuwa miongoni mwa wabunge wachache vijana kwenda nje ya Tanzania kushiriki mkutano mkuu wa dunia wa wabunge vijana. (MZEE WA MATUKIO DAIMA)
|
No comments:
Post a Comment