Joyce Kasiki, Dodoma
KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Abdulrahaman Kinana amewaomba
makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa nchini kufanya maandalizi mazuri
kwa kuteua wagombea wazuri wanaokubalika,wanaopendwa na wanaoheshimika
katika jamii ili chama kiweze kushinda kwa kishindo katika chaguzi
zijazo.
Kinana
alisema hayo mjini Dodoma wakati akifunga semina ya siku ya moja ya
sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa na makatibu hao.
Alisema
kuwa, tukishinda vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa watakuwa
wamejenga msingi mzuri kwa ajili ya uchaguzi mwaka ujao ambapo ushindi
huo huo utasaidia ushindi mwingine mkubwa zaidi wa madiwani,wabunge na
rais mwaka ujao.
Vile
vile alisema , yeye binafsi anaamini mwaka ujao pia ushindi ni kwa CCM
kutokana na kazi nzuri inayofanywa na watendaji na viongozi wa chama na
kuwaomba kujtahidi kadri ya uwezo wao kuongeza juhudi maarifa na
ufanisi.
Kinana
alisema kuwa mwaka 2009 katika uchaguzi wa seriklai za mitaa ushindi
wa CCM ulikuwa ni kwa asilimia 96 ambapo asilimia 4 zilizobaki
waligawana vyama vya upinzani kama sehemu ya wao kupumulia hivyo
anaamini hawatapata asilimia zaidi ya hizo walizopata.
Akielezea
kuhusu ziara zake anazozifanya katika mikoa mbalimbali hapa nchini
amesema ameridhishwa na maandalizi yaliyopo mikoani na wilayani hivyo
hana sababu ya kutokuwa na imani kwamba ushindi kwa CCM utakuwa mkubwa
sana.
Amesema
mpaka sasa imebaki mikoa 8 ambapo mpaka mwezi februari mwakani atakuwa
amemaliza mikoa yote nchini lengo likiwa ni kuimarisha chama,
kusukuma,kusimamia, kuhimiza utekelezaji wa ilani na ushindi katika
uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment