Mvella mwenye suti ya michezo siku moja kabla hajahukumiwa |
MAHAKAMA
ya Mkoa ya Iringa jana imemtia hatiani Mkurugenzi wa Sheria na Utawala wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Eliud Mvella baada ya kupatikana na makosa
manne ya kuendesha biashara ya bima bila kibali.
Mvella
aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi Mkoa wa Iringa kabla ya
kutimkia CCM katika miaka ya karibuni na kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) alihukumia miaka sita au kulipa faini ya Sh
Milioni 3 baada ya kupatikana na hatia ya kutenda makosa hayo.
Mvella
aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa
(IRFA) alikwepa kutumikia kifungo cha miaka sita jela baada ya
kufanikiwa
kulipa faini ya Sh Milioni 3 iliyolipwa kupitia risiti namba 3425607.
Mvella
ambaye mjini hapa anajulikana zaidi kwa jina la Mahanji alifikishwa katika
mahakama hiyo akituhumiwa kwa kosa la kwanza la kuendesha biashara ya bima bila
kibali, pili kufanya shughuli za bima bila usajiri, tatu kuuza stika za bima za
magari na kava noti bila kibali na nne kutoa risiti za bima bila kibali.
Akitoa
hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Ruth
Massam alisema Mahanji alitenda makosa hayo Mei 25, 2013 katika jengo la Higlands
hall kwa kutumia kampuni ya bima hewa iliyojulikana kama Emock.
Alisema katika kosa la kwanza, mahakama hiyo imemtia hatiani
Mvella na imempa adhabu ya kifungo cha miaka miwili gerezani au faini ya Sh
Milioni moja.
Kwa
mujibu wa hakimu huyo, Mvella amehukumiwa miaka miwili gerezani au faini ya
Shmilioni moja kwa kosa la pili na kifungo cha miaka miwili au faini ya Sh
Milioni moja kwa kosa la tatu na nne.
Kwa kupitia kampuni hewa ya bima ya Emock, Mvella alitenda
makosa hayo kwa kutumia kampuni ya Bima ya Mwananchi yenye makao yake makuu
Arusha wakati hakuwa mwajiliwa wa kampuni hiyo.
Alisema mshakiwa alikutwa na vifaa vya kampuni hiyo kwenye
ofisi iliyopo jengo hilo la Highland.
Hata
hivyo ofisi hiyo haikuwa na kibao cha jina la
kampuni lakini risiti zake zilikuwa zikionesha kuwa inafanya kazi za
Kampuni ya Bima ya Mwananchi.
Alisema Mvella alikuwa amewaajiri wanawake wawili kwa ajili
ya utoaji wa huduma hizo za bima kwa kupitia kampuni hiyo hewa ya Emock.
Wakili wa Serikali Alex Mwita aliiomba Mahakama hiyo
iangalie namna ya kumpunguzia adhabu mshitakiwa huyo kwa kuwa hajawahi kutenda
kosa lolote.
Hakimu alitoa fursa kwa wakili wa utetezi, Erick Nyato
ambaye alimwachia mshitakiwa ajitetee mwenyewe.
Mvella alisema anaomba mahakama impunguzie adhabu kutokana
na kuwa na ndugu wanaomtegemea akiwemo mama yake mzazi ambaye ana umri mkubwa
na watoto wanaosoma shule na vyuo.
Alisema pia anafanya kazi za kijamii kupitia shirika la
IYODEA (Iringa Youth Development Association). (BONGOLEAKS)
No comments:
Post a Comment