Kamanda wa Polisi mkoani
Iringa (RPC),Ramadhani Mungi
Na Friday Simbaya,
Iringa
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lugalo ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasiofahamika kisha kupora pikipiki yake ambayo haijafahamika namba za usajili.
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lugalo ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasiofahamika kisha kupora pikipiki yake ambayo haijafahamika namba za usajili.
Kamanda wa Polisi mkoani
Iringa (RPC),Ramadhani Mungi amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake leo kuwa
Salehe Khamis (18) aliuawa tarehe 06/10/2014 majira ya saa 6:15 usiku katika
Kitongoji cha Kikungwe Igumbilo, Kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa.
RPC alisema kuwa chanzo
cha mauaji hayo ni pamoja na kuwania mali, ambapo hata hivyo, watuhumiwa
wanatafutwa na jeshi la polisi.
Wakati huohuo, Jeshi la
Polisi mkoani Iringa linamshikilia dereva mmoja wa lori aina ya Isuzu kwa
kusababisha kifo cha mtembea kwa miguu huko katika Kijiji cha Itimbo Kata ya
Ihimbo, Tarafa ya Kilolo mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Iringa Ramadhani Mungi alimtaja marehemu kuwa ni Linus Mwirafi (45) mkazi
Kijiji cha Itimbo aliyedondokewa na lori hiyo baada ya kupinduka.
Alisema kuwa gari hilo
lenye namba za usajili T 244 CNK aina ya Isuzu likiendeshwa na Yoktani Kikula
(25) mkazi wa Ipogolo lilipunduka na kumdondokea mtembea kwa miguu huyo na
kusababisha kifo chake papo hapo.
RPC alisema kuwa tukio
hilo lilitokea mnamo tarehe 05/10/2014 majira 06:00hrs katika kijiji cha Itimbo
wilayani Kilolo, mkoani Iringa, na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
mwendokasi na dereva amekamatwa.
No comments:
Post a Comment