Kaimu Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya,
Mhandisi Masuka Nkina (wa kwanza kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu
ya utendaji kazi wa mizani ya Nkangamo katika barabara ya Tunduma – Laela- Sumbawanga.
Utendaji wa mizani hiyo ni kwa kutumia kompyuta ambapo mteja anachapishiwa
risiti yake hapo hapo inayoonyesha taarifa zake zote. Kama mzigo utakuwa
umezidi pia risiti hiyo itaonyesha faini anayotakiwa kulia.
Mhandisi Julius Isoka ambaye ni Mhandisi
Mshauri wa Barabara ya Tunduma-
Sumbawanga kutoka kampuni ya Nicholous Odweyer akiwaelezea timu ya ukaguzi wa
miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao wanatembelea
barabara hiyo jinsi ambavyo daraja linasukwa kutoka chini mpaka juu. Barabara hii inajengwa kwa ufadhili wa Watu wa
Marekani chini ya Mradi wa Milleniam
Challenge (MCC).
Daraja la Kashahanzi moja ya daraja kubwa na linalojengwa kwa umahiri mkubwa
katika barabara ya Tunduma –Sumbawanga. PICHA ZOTE NA JOYCE MKINGA
No comments:
Post a Comment