Monday, 20 October 2014

NHC yatumia zaidi ya shilingi milioni 700 kusaidia miradi








Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetumia jumla ya shilingi milioni 731,360,000/=kusaidia miradi ya vijana ya kufyatua tofali nchini.



Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano wa NHC, Bi Suzan Omari wakati wa Kikao kazi cha MaafisaVijana kilichofanyika hivi karibuni mkoaniTabora.


Bibi Suzan amefafanua kuwa fedha hizo zinahusisha ununuzi wa mashine uliyogharimu shilingi 297,000,000/=, mafunzo ya wakufunzi yaliyogharimu shilingi 47,000,000/= na uwezeshaji mtaji wa kuanzia kazi za vikundi vya vijana kufyatua matofali shilingi 81,500,000/=.


Ameongeza kuwa matumizi mengine kuwa ni usambazaji wa mashine uliyogharimu shilingi 30,000,000/=, uhakiki wa ubora wa mashine uliofanywa na wataalamu kutoka VETA shilingi 6,400,000/=, fedha za kununulia vifaa vya mafunzo katika kila halmashauri vilivyogharimu shilingi 130,400,000 na posho ya wakufunzi wa VETA ni shilingi 139,060,000/=.


Bi Suzan amewataka vijana kote nchini kutumia fursa hii kwaajli ya maendeleo yao ikiwemo na kuondokana na tatizo la kukukosa ajira. 

Amayetaka mashirka  mengine nchini kuiga mfano wa NHC ili kunusuru nguvu kazi hii kubwa.


Kwa upande mwingine, Meneja wa Huduma kwaJamii wa NHC, Bw, Muungano Saguya amesema kuwa wadau zikiwemo Halmashauri, Maafisa Vijana wa Mikoa na wilaya kwa kushirkiiana na mamameneja wa mikoa wa NHC wathamini mradi huu kwa kufuatilia ufanisi wake ili mradi huo uwe endelevu.


Ameongeza kuwa mradi ukiwa endelevu na kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, bajeti itaongezeka kwa mwaka wa fedha ujao ilikusaidia zaidi mradi huo kwa vijana.


Naye Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Tabora, Bw. Erasto Chilambo amesema maafisa vijana wa waunganishe vijana katika vikundi il iwatumie fursa hii kujiendeleza na kuacha kubweteka na kulalamika kwa kukosa ajira.


Aliongeza kuwa vijana wasiwe sehemu ya tatizo la ajira bali wawe watatuzi wa changamoto inayowakabili ya kukosa ajira.


Kikaohikinikikao cha kuwa kumbusha maafisa vijana majukumu yao kuwasaidia kupata uzoefu toka kwa wenzao. 

Kimeandaliwa naWizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...