Na Mwandishi Wetu, Iringa
Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo na mwingine kujeruhiwa vibaya kwa ajali wa moto na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa (RPC), Ramadhani Mungi alimtaja marehemu kuwa ni Toni Shilah (24) ambaye alikuwa ni utingo wa gari aina ya Scania mkazi wa Mbozi Masoko aliyefariki dunia baada ya gari waliokuwa wakisafiria ya mafuta kupinduka na kulipaka kwa moto.
Akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake, RPC Mungi alisema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 21.10.2014 majira ya 06:30hrs huko kijiji cha Mahenge katika Barabara Kuu ya Morogoro – Iringa Wilaya ya Iringa.
Alisema kuwa gari yenye namba za usajili T 198 CSA Scania tenki mali ya Daima Mwasamba mkazi wa Mbozi mkoani Mbeya, lililokuwa likiendeshwa na Braiton Kenneth Mwambonyika (34), ikiwa imebeba mafuta aina ya petrol na diseli lilipinduka na kuwaka moto na kusababisha kifo cha Toni Shilah na dereva wa gari kujeruhiwa vibaya na kulazwa Hospitali ya Rufaa ya Iringa.
RPC alielezea kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe na mwendokazi.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia George Makombe (22) mkazi wa Mwembetogwa Kata ya Makorogoni Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa kwa tuhuma ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bhangi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe 21.10.2014 majira ya 18:30hrs huko maeneo ya Mwembetogwa Kata ya Makorongoni Manispaa ya Iringa, ambapo Makombe alikamatwa na madawa ya kulevya aina ya bhangi gramu 70 ndani ya Rambo nyeusi na askari polisi waliokuwa doria.
No comments:
Post a Comment