Hali ya Rais Jakaya Kikwete imeendelea kuwa nzuri baada ya kuruhusiwa hospitalini na kuendelea na mapumziko. Amekuwa akiendelea na mazoezi aliyopangiwa na kufanya kazi mbalimbali za kiofisi.
Jana, Jumapili tarehe 16, Nov 2014 Rais ametembelewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe aliofuatana nao ambao wako nchini Marekani kuhudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa mabadiliko ya sheria ya ushahidi jijini Washington.
Watanzania, tuendelee kumuombea dua na kumtumia meseji za kumtakia kheri Mheshimiwa Rais na kumfariji katika kipindi hiki cha maradhi.
No comments:
Post a Comment