Monday, 17 November 2014

Siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini (HAND WASHING DAY)

Kibuyu Mchirizi kwa ajili ya kunawa mikono kwa maji safi na salama na sabuni baada ya kutumia choo.


Ofisa Afya wa mkoa wa Iringa Khadija Harouni (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu ziara maalum ya mafunzo katika Shule ya Msingi Nyololo kwa walimu wa shule hiyo pamoja na wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya Mufindi, mkoani Iringa. Shule hii ilichaguliwa kutekeleza kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira, matumizi ya maji vyooni na afya shuleni (SWASH). (PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA)


Shule ya msingi Nyololo ilianzishwa tarehe 02.01.1961 na kwa sasa inajumla ya wanafunzi 366 wakiwemo wavulana 200 na wasichana 166 na walimu waliopo ni kumi na moja.

Wiki ya usafi wa mazingira nchini ulianza tarehe 13.11.2014 na kilele kitakuwa tarehe 19.11.2014. 






 Mmoja wa maofisa afya akionesha mfano namna ya kutumia choo kwa upande wakike (urinal system).



 Mwalimu Mkuu Shule ya msingi Nyololo, Blastus Andrea Kidava (wa tatu kushoto) akitoa taarifa ya mradi wa SWASH (School Water, Sanitation and Hygiene) ambapo walijenga matundu manane ya vyoo vya wanafunzi wa kike.

Malengo ya mradi huu ni kuboresha afya za wanafunzi, walimu na jamii nzima kwa ujumla. Mradi huu pia umelenga kupunguza magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na uchafu wa mazingira, kutonawa mikono kwa maji safi na salama baada ya kutoka chooni na kutotumia choo.




No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...