Sunday, 2 November 2014

CHADEMA WAENDELEA KUHAMASISHA WANANCHI KUHUSU UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Katibu wa  CHADEMA  Wilaya ya Iringa mjini Suzan Mgonokulima (katikati) akihutubia wananchi wa  Mtaa wa Mwangata D eneo la Mapekosi katika Kata  ya Mwangata wakati mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni wenye lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza na kugombea nafasi za uongozi kama vile uwenyekiti na ujumbe  katika mtaa huo hasa akinamama.


Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Mwangata D wakijitokeza kujiandikisha majina kwa mmoja ya viongozi wa CHADEMA ili kuweza kushiriki katika mchakato wa kumpata mwenyekiti wa mtaa pamoja na wajumbe 6 kupitia chama hicho na hatimaye kuweza kushindanishwa na vyama vinge vya siasa vitakavyosimamisha wagombea wao wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa hapo tarehe 14 Desemba mwaka huu.

Katibu Mwenezi wa Chadema wa Jimbo la Iringa mjini, Baraka Kimati akiongea na wananchi wa Mtaa wa Mwangata D eneo la Mapekosi, Kata ya Mwangata wakati mkutano wa hadhara wa kuhamisha wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Desemba mwaka huu.


Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Iringa mjini, Frank Nyalusi akiongea na wananchi wa Mtaa wa Mwangata D eneo la Mapekosi wakati mkutano wa hadhara wa kuhamisha wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuongeza kuwa wasikubali kurubuni na wanasiasa kwa kwa vitu vidogo vidogo.

Mwenyekiti huyo wa wilaya ambaye pia diwani wa Kata ya Mivinjeni aliwataka wananchi hao kujiandkisha kwenye daftari la makazi la mtaa ili  wawe wapigakura halali wa mtaa huo wakati uchaguzi wa serikali za mitaa unapokuja na kuchaguza viongozi wachapakazi.







No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...