Sunday, 2 November 2014

IGP MSTAAFU PHILEMONI MGAYA ASHEREHEKEA MIAKA 85 YA KUZALIWA



Mara Baada ya Ibada katika Kanisa la Azania Front wakati wa kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya

Baadhi ya waumini mbalimbali wakiwa nje baada ya Ibada


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Mstaafu Philemoni Mgaya akiwa katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake 



Keki

Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimpongeza aliyekuwa IGP Philemoni Mgaya 

Mzee Timothy Msangi akieleza Historia fupi ya IGP Mstaafu Philemoni Msangi 

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu 

Mshauri wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira akitoa pongezi zake kwa IGP Mstaafu na kuelezea Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu 


Mshereheshaji Joe Mgaya ambaye ni Mtoto wa IGP Mstaafu Philemoni Mgaya akisherehesha




Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara akimpa mkono wa Pongezi IGP mstaafu 






IGP Mstaafu akipokea zawadi


IGP Mstaafu Philemoni Mgaya akikata keki huku amezungukwa na wajukuu wake

















WAZIRI Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya amewaomba watanzania  kuwa na tabia ya utii wa sheria, uaminifu na uadilifu katika nafasi za wanazozitumukia katika Taifa la Tanzania.

Msuya aliyasema hayo katika sherehe ye kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya iliyofanyika katika Hotel ya Protea , Court Yard jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mstaafu alieleza kuwa tabia aliyoionyesha Mgaya wakati wa utumishi wake serikalini inapaswa kuigwa na watanzania wote.

“Huyu ndiye Mtanzania halisi aliyelelewa vizuri kuitumikia nchi yake. Hana makuu, ni mkweli na mwadilifu. Akiahidi kufanya jambo fulani analitekeleza bila kuchelewa. Tunahitaji uwajibikaji wa namna hii,” Msuya alisisitiza.


Alisema kuwa Mgaya alikuwa kiongozi hodari ambaye alisimamia vyema kiapo na kazi zake na kipindi chake cha uongozi alikuwa akitoa amri zinatekelezwa mara moja.


Naye Mshauri wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira alitoa wito kwa watanzania kuendele kuunga mkono jitihada za kuendeleza maeneo mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo viwanda.


Aliwasihi wadau kutoa ushirikiano kwa kampuni yake inayosambazabia aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught ambayo inadhamira ya kujenga kiwanda cha kuzalisha bia hizo hapa nchini.

“Tunatafuta maeneo Kilimanjaro, Tanga na Bukoba ili tuweze kujenga kiwanda hapa nchini. Tumedhamilia kufanya hivyo na tutafanya,” Rugemalira alisisitiza.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira aliwashukuru wananchi kwa kukubali kujumuika pamoja katika hafla hiyo na kumwomba Mzee Mgaya aendelee kuwapa mwongozo wa namna ya kuenenda katika maisha.


Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa aliwaomba watanzania kuwa na moyo wa unyenyekevu na kujitolea kulitumikia taifa katika utumishi wao kama ilivyokuwa
kwa IGP mstaaafu Mzee Mgaya.

Wageni wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara, Katibu Mkuu Msaaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Bakari Mwapachu, Balozi Antoni
Nyaki na wazee wengine maarufu kama Timothy Msangi.






kawaida

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...