Monday, 24 November 2014

KABATI ATAKA WANAWAKE WAJITOKEZE KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI








MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) amewakata wananchi kutokubali kudanganywa na vyama vya siasa vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) juu ya katiba inayopendekezwa na badala yake kuungana na watanzania wapenda maendeleo kuikubali katiba hiyo muda utakapofika.



Mbunge alitoa kauli hiyo wakati wa semina elekezi kwa kina mama  wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Mufindi leo baada ya kufanya semina kama hizo katika wilaya ya Iringa na Kilolo.

Alisema kuwa semina ililenga kuwajengea uwezo wa kujiamini kwa wanawake waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali za mitaa na vijijini .


Kabati alisema kumekuwepo na upotoshwaji mkubwa ambao umeendelea kufanywa na UKAWA kwa kuzunguka huku na kule kujaribu kupotosha ukweli juu ya katiba iliyopendekezwa kwa madai kuwa ni katiba ya CCM na kuongeza  katiba hiyo ulifanywa na vyama vyote na makundi maalum.


Pia alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wanasiasa wasilolitakia mema Taifa hili kwa kupotosha juu ya katiba hiyo ni sawa na kutaka kuona nchi haitawaliki na hivyo kuamua kuanza upotoshaji huo.


Alisema kuwa si kweli kama katiba hiyo iliyopendekezwa haina jambo lolote la msingi kama ambavyo UKAWA wamekuwa wakizunguka na kupotosha ila alidai kuwa ndani ya katiba hiyo kuna mambo mengi yamezingatiwa kwa ajili ya wananchi na Taifa kwa ujumla.


Akielezea kuhusu mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ,vijiji na vitongoji unaotaraji kufanyika hivi karibuni alisema kuwa upande wa mkoa wa Iringa wanawake baada ya kuhamasishwa wamejitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali za uongozi na kuwa baadhi ya maeneo wamepata kushinda kwa kishindo nafasi walivyoomba ndani ya CCM wakisubiri uchaguzi rasmi wa serikali .


Hivyo aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kujitokeza kuwapa kura zao wanawake hao waliogombea nafasi mbali mbali na kuwa imani yake kuona kunakuwa na uongozi mchanganyiko.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...