Friday, 21 November 2014

NJIA BORA YA KUOKOA MAISHA YA WATOTO NA JAMII NI KUNAWA MIKONO











Kilele cha maadhimisho ya siku ya choo duniani, siku ya unawaji mikono na wiki ya usafi Tanzania imefikia kikomo ambapo zaidi ya watu bilioni 4.5 tu ndio wanaomiliki na kutumia vyoo bora huku watu bilioni 2.5 duniani kote hasa maeneo ya vijijini hawana vyoo bora.



Katika hotuba ya Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, iliyosomwa na Mganga mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt Robert Salim, ya kufunga maadhimisho hayo Kimkoa iliyofanyika Kijiji cha Ifunda, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mwaka 2013 umoja wa mataifa ulipitisha tarehe 19 Novemba ya kila mwaka kuwa ni siku rasmi ya maadhimisho ya choo Duniani, ambapo mwaka huo huo Tanzania ilipitisha rasmi tarehe 13-19 Novemba kuwa ni wiki ya usafi Tanzania pamoja na siku ya kunawa mikono Duniani sambamba na siku ya choo Dunia.




Taarifa zinaonyesha kuwa matumizi ya choo bora na kunawa mikono kwa sabuni ni moja ya njia bora ya kuokoa maisha ya watoto na jamii nzima kwa ujumla, kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni kupunguza kuenea kwa magonjwa ya kuhara na manufaa yake ni ya muda mrefu kwa afya na ustawi wa watoto na jamii kwa ujumla.



Takwimu zinaonyesha kuwa matumizi ya choo bora hupunguza magonjwa ya kuhara kwa asilimia 32 na kunawa nikono kwa sabuni hupunguza magonjwa hayo kwa asilimia 50, ambapo Takwimu za mwaka 2013 zinaonyesha kuwa watoto 1000 wanakufa kwa kila siku moja duniani kote kutokana na magonjwa ya kuhara.


Aidha baadhi ya taasisi zilipatiwa zawadi mbalimbali kutokana na uboreshaji wa huduma za maji, afya na mazingira ikiwa ni pamoja na shule ya msingi Nyololo, ambapo Manispaa ya Iringa ilipata zawadi ya kuweza kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya mkusanyiko, huku Kitongoji cha Mpwapwa kilichopo kijiji cha Kihanga kilipata zawadi ya kuwa kitongoji kisichotupa kinyesi ovyo.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...