Tuesday, 11 November 2014

TUPSE CHA FUNGUA TAWI CHUO KIKUU CHA IRINGA (IUCO)

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE), Edison Kivelege (kulia) akionesha kadi ya chama hicho kwa wanachama wapya wa tawi la chuo kikuu cha iringa wakati mkutano uliofanyika chuoni hapo hivi karibuni. Wa pili toka kulia ni Katibu wa kanda wa TUPSE, Ashura Mikidadi Ngaga na wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa kanda hiyo Elias Mussa Mwinyi ambaye pia mlinzi wa chuo hicho. 



Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE), Edison Kivelege akifurahia jambo na mmoja wa viongozi waliochaguliwa katika tawi jipya la chama hicho muda mfupi baada ya kumalizika kwa uchaguzi na kukabidhiwa kadi kwa ajili kuwakabidhi wenzie.


Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE), Edison Kivelege akitoa ufafafuzi juu ya chama kinavyoweza kuwasaidia endepo watapata matatizo na mwaajiri wao, na kuongeza kuwa chama hicho ni chombo cha usuluhisho (mediation). (Picha zote na Friday Simbaya)

No comments:

ASAS AWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU VURUGU ZA UCHAGUZI

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas , amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchagu...