Mwenyekiti
wa mtandao wa vyombo vya habari vya kijamii Tanzania (COMNETA) ambaye
pia ni Mkurugenzi wa redio FADECO ya wilayani Karagwe, Bw. Joseph
Sekiku, akimtambulisha mgeni kutoka nchini Uingereza kwa wamiliki wa
redio za jamii katika mkutano uliojadili masuala ya kiufundi uliofanyika
mwishoni mwa juma Chuo kikuu huria.(Picha zote na Zainul Mzige).
Na Mwandishi wetu
Kampuni
Broadcast warehouse ya Uingereza imesema ipo tayari kusaidia radio za
jamii ambazo kwa sasa zinakabiliwa na changamoto nyingi za uendeshaji
hasa katika masuala ya kiufundi kwenye teknolojia ya utangazaji ya
digitali.
Mtaalamu
wa kampuni hiyo, Brendan Lofty ambaye aliwasili nchini kwa ajili ya
mkutano na wanachama mtandao wa vyombo vya habari vya kijamii Tanzania (COMNETA) amesema ipo haja ya kuangalia mfumo wa pamoja wa kiufundi ambao utafanya redio hizo kuwa endelevu.
Alisema
anafahamu umuhimu wa radio hizo za jamii ambazo zinaelekeza nguvu
kushughulikia matatizo ya jamii kuliko redio za biashara na kusema yupo
nchini kuhakikisha anajibu kiu ya wamiliki hao inamalizika na
wanaendelea na majukumu yao.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wanachama mtandao wa vyombo vya habari vya
kijamii Tanzania (COMNETA) ambao ni mameneja na wamiliki wa redio za
jamii nchini waliohudhuria mkutano wa siku moja uliojadili masuala ya
kiufundi uliofanyika mwishoni mwa juma Chuo kikuu huria.
Alisema
katika kuelekea uchaguzi na hasa baada ya TCRA kutoa hadidu za
kuzingatiwa inafaa wahusuka wote kuwa katika hali ya kujiamini kwa kuwa
na utaalamu unaotakiwa katika kuendesha redio hasa masuala ya kiufundi.
“Nimekuja kuwatoa hofu, tutaelezana na kushauriana namna bora ya kusaidiana kufikia kuwa na redio bora” alisema Lofty.
Alisema
katika utafiti wake amebaini kwamba radio za jamii nchini zina kazi
kubwa na ya maana kuliko zile za kibiashara na kwamba zipo zenye hali
bora zaidi kiufundi kuliko zilizopo Ulaya.
Naye
Mwenyekiti wa Comneta, Joseph Sekiku akielezea mkutano huo amesema
umeitishwa makusudi kwa ajili ya kupata uzoefu wa mtaalamu huyo wa
Uingereza kutokana na redio nyingi kuwa na matatizo ya kiufundi kwenye
digitali .
Alisema
kutokana na makampuni yaliyouza vifaa mengi kutokuwa na program za
kufuatilia vifaa vyao, redio nyingi zimejikuta zikilazimika kununua
vifaa vingine walivyonavyo vinapopata hitilafu na hivyo kuongeza mzigo
wa uendeshaji.
Alisema
wakati Comneta inataka kuwa na uwiano wa ubora wa vifaa na wauzaji wake
wameona ni vyema kumuita mtaalamu huyo wa Uingereza ambaye pia kampuni
yake inauza vifaa vya radio na digitali kuona namna bora ya
kushirikiana.
Aidha
alisema hali hiyo imesababishwa na mahitaji halisi ya kuzifanya redio
hizo kuwa endelevu na kuendelea kuhudumia jamii hasa kuelekea katika
uchaguzi.
Alisema
nyingi ya radio hizo hazinahifadhi ya vitu vinavyorushwa kwa siku,
hivyo kama masuala hayo yakitatuliwa suala la kufuatilia haki katika
mashauri na TCRA yanaweza kuwa na nafuu zaidi.
Mtaalamu
kutoka kampuni ya Broadcast warehouse ya Uingereza, Bw. Brendan Lofty,
akifafanua masuala ya kiufundi yanayohusu redio na programu zake kwa
ujumla kwenye mkutano wa siku moja na wanachama wa COMNETA.
Meneja
wa kituo cha redio jamii TUMBATU FM, Bw. Ali Khamis akielezea
changamoto mbalimbali za kiufundi wanazokumbana nazo kwenye kituo chake
wakati wa mkutano huo na Mtaalamu wa Kampuni ya Broadcast warehouse ya
Uingereza, Bw. Brendan Lofty (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa redio jamii Uvinza Fm, Alhaji Ayubu Kalufya akiuliza swali kwa mtaalamu huyo Bw. Brendan Lofty(hayupo pichani).
Mtaalamu
kutoka kampuni ya Broadcast warehouse ya Uingereza, Bw. Brendan Lofty
akibadilishana mawazo na baadhi ya wanachama wa mtandao wa vyombo vya
habari vya kijamii Tanzania (COMNETA) wakati wa mkutano huo wa siku moja
uliofanyika Chuo Kikuu Huria mwishoni mwa juma. (EDITED BY FRIDAY
SIMBAYA)
No comments:
Post a Comment