Wakili wa kujitegemea Charles Paul Lawisso akiwaapisha wenyeviti na wajumbe kamati za mitaa manispaa ya iringa katika ukumbi wa orofea.
Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya iringa Augustno Nyenza
wajumbe wakisaidiana kujaza fomu za kiapo ndani ya ukumbi
WENYEVITI wa
serikali za mitaa walichaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wa serikali za
mitaa katika manispaa ya iringa wameapishwa jana kwa kupewa onyo kali na wakili
wa kujitegemea Charles Pau Lawisso kwamba atakayeenda kinyume atachukuliwa
hatua kali za kisheria.
Lawisso ambae ni wakili wa kujitegemea alitoa
onyo hilo wakati wenyeviti hao wakiapishwa mjini iringa.
“Wapo
viongozi watakaosema sera ya chama chetu hairuhusu wananchi kuchangia miradi ya
maendeleo na ama wapo watakaozuia michango kwa lengo la kulinda na kutetea
wapiga kura wao…kitendo hicho kitakiwa kinakwenda kinyume na sheria za nchi na
hivyo ukibainika hatua zitachukuliwa dhidi yako.”alisema lawisso.
Aliongeza kuwa kazi za wenyeviti hao kuwa ni
pamoja na kufuatilia miradi ya maendeleo katika mtaa husika na kutekeleza
maagizo kutoka ngazi za juu yaani kata na Manispaa.
Lawisso wakati akitoa onyo
hilo limekuja sera ya chadema kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa ni
kuhakikisha inazuia michango isiyoyalazima kwa wananchi wake, kutochangisha
michango kwa ajili ya huduma za kijamii ikiwamo utoaji wa barua za dhamana na
mikopo kutoka katikataasisi mbalimbali.
Pia alitaja kazi za
wenyeviti hao kuwa pamoja na kufuatilia na kusimamia miradi ya maendeleo
watakuwa na jukumu la kusuluhisha migogoro inayotokea katika mitaa yao ambayo
maamuzi yake hayahitaji kufika ngazi za juu.
Nae kaimu mkurugenzi wa manispaa ya iringa Augustno
Nyenza alisema kuanzia sasa wenyeviti na wajumbe waliochaguliwa na viongozi wa
serikali watakaosaidia na ofisi yake kutekeleza masuala ya serikali ya Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania.
“Leo mmeapa kulitumikia
taifa na wananchi kwa ujumla na baada ya kiapo hiki mnapaswa kutambua kuwa kazi
mmeanza rasmi na leo hii mmekuwa viongozi wa kamili wa serikali ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania,mtafanya kazi zenu kwa kushirikiana na watendaji wa
serikali za mitaa,kata na Halimashauri ya manispaa katika utekelezaji wa majukumu
yake ya kila siku”alisema Nyenza.
Katika uchaguzi huo uliofanyika hivi karibuni
jumla ya wenyeviti 192 wa manispaa ya iringa na wajumbe 960 walitarajia kula
kiapo cha utii kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa shughuli za kiserikali katika
mitaa yao.
Uchaguzi huo uliofanyika
ni kwamba jumla ya 192 huku chama cha mapinduzi CCM kikijinyakulia viti 126 na
chadema 64 na CUF viti viwili.
No comments:
Post a Comment