Sunday, 11 January 2015

Msambatavangu: Vijana msikubali kutumika kisiasa...!

Afisa Kilimo waManispaa ya Iringa, Robert Semaganga akionyesha mfano ya namna ya kuchimba mashimo ya kupanda mbegu za alizeti katika shamba la vijana lililopo kijiji cha Kising'a wilayani Iringa jana.

Mpishi akipika chakula kwa ajili ya vijana waliokwenda kupnada mbegu za alizeti katika shamba la vijana lililopokijiji cha Kising'a wilayani Iringa jana.

Vijana wakishuka kwenye gari baada ya kufika shambani kwa ajili ya kupanda alizeti katika shamba la vijana lililopo kijiji cha Kising'a wilayani Iringa jana. 


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akishiriki kupanda alizeti katika shamba la vijana lililopo kijiji cha Kising'a wilayani Iringa jana. 



Mpishi akimuandaa ndege aina kwale aliyenaswa kwenye mtego katika shamba la utafiti la uyole ambapo vijana zaidi ya 100 kutoka zote za manispaa ya iringa walishiriki kupanda alizeti katika shamba la vijana lililopo kijiji cha Kising'a wilayani Iringa jana. 



Vijana wakifungua mfuko wa mbegu za alizeti kwa ajili ya kupanda.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa shamba la utafiti la uyole kabla ya kushiriki kupanda alizeti katika shamba la vijana lililopo kijiji cha Kising'a wilayani Iringa jana.  



Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu amewaasa vijana kutotumika katika masuala yasiyo na tija kwa maendeleo ya Taifa.

Mwenyekiti huyo alisema hayo jana katika Kijiji cha Kising’a kilichopo Jimbo la Isimani watika akishiriki katika zoezi la ukupandaji wa mbegu za alizeti kwa kushirikana na vijana katika shamba lililotolewa na serikali kwa vijana.

Alisema kuwa imefika wakati sasa vijana wajitambue na kujiongeza na kukataa kutumika kisiasa na wanasiasa wenye maslahi binafsi kwa ajili ya kujijenga kisiasa.

Alisema serikali imetenga maeneo kwa ajili ya mashamba ya vijana kujishughulisha na mambo ya kiuchumi kikiwemo kilimo na hatimaye kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

“Vijana watakiwa kujiangalia na maisha yao wenyewe wanatakiwa kuona mbali kwa kuangalia maisha ya baadaye na sio kukumbali kutumika kisiasa. Wanatakiwa wajiue kwamba wanatakiwa kuwa wazalishaji mali na hatimaye kuondokana na umasikini ya kipato,” alisema mweneyekiti.

Alisema kuwa kuna wanasiasa wanadanganya vijana kwa manufaa yao binafsi na kuongeza kwa kufanya hivyo ni kutengeza bomu la vijana linalosibiri kulipuka muda wowote.

Aliwakumbusha pia wanasiasa  kutowadanganya vijana kwa sababu wakija kugundua kwamba wanaganganywa inakuwa  wakakata tama na kama Nigeria ambako vijana watumika kisiasa. (political thug mafias). 

 Zaidi ya vijana 100 kutoka katika kata mbalimbali ya Manispaa ya Iringa walishiriki katika zoezi la kupanda alizeti katika mashamba yalipewa na serikali kwa ajili ya vijana.

Mashamba hayo yalipewa na Manispaa ya Iringa kutoka shamba la utatifi la uyole yaliopo Kijiji cha Kising’a wilayani Iringa.

Alisema kuwa serikali ilitoa eneo la kulima pamoja na mbegu za alizeti na kwa upande wake alitoa mchango wakulima mashamba hayo kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika kilimo kwa kutekeleza ilani uchaguzi ya ya CCM mwaka 2010 ya kuwawezsha vijana.

Hivi karibuni serikali iliaagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya kilimo kwa ajili ya vijana ili kwawezesha katika kilimo na kuwafanya vijana mbinu za  kujitegemea.

Hata hivyo zaidi ya akari 90 zilipandwa mbegu za alizeti ambapo zitakagawiwa akari mbili mbili kwa  vijana kumi  kumi.

Kwa upande wake, Afisa Kilimo wa Manispaa ya Iringa, Robert Semaganga ambaye pia ni msimamizi wa program ya kusaidia vijana katika manispaa alisema vijana ni vema wakajishughulisha katika shughuli za kililmo.

Alisema serikali ametoa fursa kwa vijana kwa kutoa maeneo kwa ajili ya vijana kujishughulisha na uzalishaji mali ambapo eneo lililotoa na shamba la utafiti Uyole ni akari 150 na mpaka sasa ni eneo la akari 90 zimelimwa na kupandwa zao la alizeti.

Alisema kuwa aina ya mbegu ya alizeti ya rekodi ambayo ni nyeusi  imepandwa katika mashamba hayo ambayo inastahimili ukame  pamoja na kutoa mavuno mazuri.

Afisa kilimo huyo alisema kuwa mbegu hiyo inatoa mavuno mazuri ukilinganisha na mbegu zingine za alizeti kwa mfano, akari moja ya mbegu ya rekodi inatoa maroba kati ya nane hadi kumi na mbili (12).

Alisema kuwa halmashauri iliazimia kuwasaidia vijana katika  kilimo ambapo ilitoa mbegu ya alizeti kilo 500 pamoja kusaidia kulima mashamba hayo.
 




No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...