Saturday, 10 January 2015

WANAUME ZAIDI LAKI MOJA NA TISINI KUTAHIRIWA MKOANI IRINGA


Mkoa wa Iringa una lengo la kutahiri wanaume 191,999 mwaka huu  na hadi kufikia Septemba mwaka jana jumla ya wanaume 147,620 sawa na asilimia 76.9 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 wametahiriwa.


akiwasilisha taarifa ya utakelezaji wa shughuli za mapambano dhidi ya ukimwi na dawa za kulevya jana watika kikao cha kamati ya ushauri mkoa wa Iringa (rcc),  mtaalamu wa magojwa ya ngono mkoani Iringa Dkt. Paul Luvanda alisema kuwa kiwango cha tohara mkoani iringa kimeongezeka.

Dkt. Luvanda alisema kuwa katika utafiti uliofanyika mwaka 2011/2012 unaonyesha kuwa kiwango cha tohara kimeongezeka  kutoka asilimia 37.7 mwaka 2007/2008 hadi asilimia 60 mwaka 2011/2012.

Aidha, alisema huduma ya tohara kwa wanaume katika mkoa zinatolewa katika vituo kumi na mbili (12) ikiwemo hospitali ya rufaa ya mkoa, kituo cha afya ngome (manispaa ya iringa), hospitali teule ya tosamaganga (halmashauri ya iringa), hospitali teule ya ilula (halmashauri ya kilolo) na hospitali ya wilaya ya mufindi na pia kwa njia ya kampeni.

Mkoa una mradi maalum wa tohara ya watoto wachanga (siku 2 mpaka siku 60). Mradi huu ni katika jihudi za kusaidia magonjwa ya mkojo kwa watoto, magonjwa ya ngozi ya sehemu ya uume, kwa  wasafi kwa urahisi zaidi na maandalizi ya kupunguza VVU atakapoweza kufanya tendo la kujamiana ukubwani.

Alisema kuwa huduma ya tohara kwa watoto hao wachanga wanaume zinatolewa katika vituo vifuatavyo; hospitali ya rufaa ya mkoa, kituo cha afya ngome na zahanati igumbilo (manispaa ya iringa), hospitali teule ya tosamaganga, hospitali teule ya ilula na kituo cha afya kidabaga (kilolo) na hospitali ya wilaya ya mufindi, pia kwa njia ya kampeni.

Mradi huu umeanza mwezi wa julai, 2013 hadi kufika mwezi septemba mwaka 2014 jumla ya waoto wachanga 2,200 wametahiriwa.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...