Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsikiliza mwanafunzi wa shule ya sekondari Kiwere akifanya vitu vyake kwa kushirikiana wanafunzi wenzake katika maabara ya kemstri alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa shuleni. Pinda leo alikagua ujenzi wa maabara na kufungua nyumba nne za walimu wa shule
hiyo zenye uwezo wa kubeba familia nane, halmashauri ya wilaya ya iringa katika jimbo la kalenga.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua mradi wa umwagiliaji pamoja na mashamba ya wakulima wa mpunga wa kijiji cha magozi, halmashauri ya wilaya iringa jimbo la isimani, akifuatana na mkuu wa mkoa wa iringa amina masenza akifuatia na kaimu mkuu wa wilaya ya iringa Gerald Guninita ambaye pia ni DC wa kilolo.
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda amewataka watanzania hasa wana chama wa chama cha mapinduzi (
CCM)kuwa na subira katika kumpata mwanachama atakayefaa kusimama kugombea urais
kupitia CCM mwaka huu.
“Kuwa tayari
wengi sana wamejitangaza wazi wazi na wengine wamejitangaza kimya kimya kutaka
kugombea Urais na kuwa yote heri ila chama kina utaratibu wake. Itafika wakati
ambao kila chama kitasema huyu ndie mtu wetu ambaye atapambanana vyama vingine
...tunachosema sisi huyo atakayependekezwa ndie atakuwa mgombea wetu,"alisema
Waziri Pinda Waziri
Pinda alitoa
kauli hiyo jana wakati akiwahutubia wakazi wa tarafa ya Pawaga baada ya
kuzindua skimu ya umwagiliji itakayowanufaisha wakazi wa vijiji vitatu kikiwemo
cha Magozi,Ilolompya na Mkombilenga uliogharimu zaidi ya Tsh bilioni 1.6 fedha
kutoka kwa wahisani na serikali.
Alisema kuwa
utaratibu wa ndani ya chama ambacho wao ni watawala na wanaoendelea kuyafanya
maendeleo yanaonekana watalazimika kumuunga mkono atakayeteuliwa na wale wote
ambao hawajateuliwa watamuunga mkono atakayeteuliwa kwa makundi yote kuvunjwa
na kuwa na Kundi moja pekee.
Baada ya mgombea wa chama tawala kupatikana
jukumu kubwa ni kuwaomba wapenzi wao wote kumchagua huyo aliyeteuliwa na chama.
Hivyo Waziri
Pinda aliwataka wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye
daftari la kudumu la wapiga Kura.
Alisema kuwa
zoezi hilo ambalo litawahusu wale wote wenye miaka kuanzia 18 na kuendelea
linataraji kuanza mwezi huu katika Mkoa wa Njombe na kuwa kila kata zoezi hilo
litadumu kwa muda wa wiki mbili ama tatu .
"
Nawaombeni kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na pia kuipigia kura katiba
inayopendekezwa muda ukifika sisi tunaamini ni katiba bora ambayo imegusa
makundi yote yakiwemo ya wafugaji na wakulima pamoja na makundi mengine," alisema
Pinda.
Kuwa wapo
wapotoshaji ambao watafika na kuwadanganya juu ya katiba hiyo inayopendekezwa
na wasiwasikilize na kuongeza kuwa kazi kubwa imefanyika katika kuandaa katiba
hiyo inayopendekezwa mbali ya wao (UKAWA) kutoka nje wakati wa bunge hilo la
katiba lakini wajumbe waliobaki walifanya kazi nzuri ya kuandaa katiba hiyo
inayopendekezwa hivyo kuwaomba wananchi kuipigia kura.
Katika hatua
nyingine Waziri mkuu Pinda amewataka wakulima wa mpunga Pawaga katika kuepuka
na migogoro kati yao na wafugaji kuweka utaratibu wa kukusanya majani ya mpunga
na kuyapeleka majumbani kwao ili wafugaji wapate kununua kuliko kuyaacha
mashambani na kuwafanya wafugaji kuingiza mifugo yao mashambani.
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda yupo katika ziara ya siku tano mkoani Iringa kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo na baada ya hapo ataelekea mkoani Mbeya kuendelea na
ziara.
No comments:
Post a Comment