Edson Mwesigwa, 25 akiwa dukani siku ya mwisho.
MUUZA duka ya rejereja, Edson Mwesigwa miaka 25 mkazi wa Wilaya ya Misenyi mkoani Bukoba amedaiwa kumwibia mwajiri wake
fedha taslimu milioni 2.6 mauzo ya MPesa
usiku wa kuamkia tarehe 26/02/2015 na kisha kutokomea kusikojulikana.
Kijana huyo mwenyeji wa Kijiji cha Kigarama, Kata ya Kanyigo , Tarafa ya Kiziba wilayani Misenyi, Mkoa wa Kagera amedaiwa kumwibia mwajiri wake mauzo
ya Mpesa nyumbani kwake Mtaa wa Wilolesi, Kata ya Gangilonga katika Manispaa ya
Iringa mkoani Iringa.
Akiongea na Nipashe jana (IJUMAA) mwajiri huyo Edina
Byemerwa mkazi wa Mtaa wa Wilolesi, Kata ya Gangilonga katika
Manispaa ya Iringa alisema siku ya Ijumaa tarehe 26 mwezi Februari mwaka huu
aliamka kama kawaida na kwenda kumgongea mtumishi huyo ili awahi kwenda dukani
bila mafanikio.
Alisema kuwa alipoona kijana wake wa ndani hafungui
mlango ndipo alipolazimisha kufungua mlango na kukuta chumbani kwake hakuwepo
mtu na kwenda kumwambia mtoto wake ambaye wakati huo alikuwa anaoga bufuni na
kusema mbona kijana (Edson) hayupo.
Kijana wake ambaye ni mtoto wake ambaye alikuwa
anaoga alisikika akisema akimwambia mama yake kuwa hapo sebuleni kuna begi lina
hela ya mauzo ya Mpesa aliyeuza jana angalia kama lipo.
Lakini mama huyu alipoangalia vizuri sebuleni alikuta
begi halionekani ndipo alirudi tena chumbani kwa mtumishi wa ndani kuchunguza na
kukuta amebeba kila kitu kilichokuwa chake.
“Niliamka asubuhi na mapema na kwenda kumwamsha kijana
wangu muuza duka la rejareja pale mjini na kukuta kijana chumbani kwake
hakuwepo, ndipo nilirudi sebuleni tena kumuuliza mtoto wangu ambaye alikuwa
anaoga bafuni kwamba mbona Edson hayupo chumbani kwake! Mtoto akaniambia
niangalie begi hapo mezani lina mauzo ya Mpesa ya jana kama lipo na kukuta kweli begi
halipo…” alisema mwajiri huyo.
Hata hivyo, mwajiri huyo alisema wameripoti tukio hilo
katika Kituo cha Polisi Iringa kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba
IRI/RB/1678/2015 na polisi wameahidi kumpa ushirikiano.
Aliongeza kuwa kijana wa kazi (Edson )alitokea mkoani
Bukoba nakuja kufanya kazi ya duka la rejareja mnamo tarehe 23/12/2014 na kwa
sasa ni zaidi ya wiki tatu zimepita tangu mtumishi huyo atoweke nyumbani hapo.
“Kijana huyo alikuwa anauza vitu vya dukani na mtoto
wangu wa kiume alikuwa anasaidia kuuza Mpesa hapo hapo dukani.
Alisema kuwa mtu yeyote atakayemuona atoe taarifa
kituo cha polisi au kwa namba ya simu 0754917217 na kuongea kuwa donge nono litatolewa
kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa kijana huyo.
No comments:
Post a Comment