mwanahabari frank kibiki , aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec akiwa na watoto waliofanyiwa ukaliti wa kijisia pamoja mkuu wa kituo cha matumaini centre
mwandishi wa habari wa gazeti la mzalendo na uhuru TUMAINI MSOWOYA KIBIKI akiwa na watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia
mwandishi wa habari wa gazeti la mzalendo na uhuru TUMAINI MSOWOYA KIBIKI akiwa na watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia pamoja na mkuu wa kituo cha matumaini centre.
na fredy mgunda,iringa
Ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike ndio inaonekana kuwa sababu ya mkoa wa iringa kuzalisha wafanyakazi wengi wa kazi za ndani
akizungumza na blog hii mwanahabari frank kibiki , aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec.amesema kuwa watoto wengi wa kike hawapewi nafasi ya kwenda kusoma kutokana na tamaduni potofu hivyo waandishi wa habari tunatakiwa kuungana kuwapigania watoto hawa.
Aidha KIBIKI amewataka wananchi wa mkoa wa iringa kushirikiana na mkuu wa kituo cha matumaini centre ili kuwasaidia watoto wa kike ambao wanaishi katika kituo hicho.
lakini KIBIKI amewaomba viongozi mbalimbali na waandishi wa habari kupaza sauti zetu ili kukomeshakabisha suala la ukatili wa kijinsia ambao bado unaendelea hapa mkoani kwetu.
Wananchi mkoani iringa wametakiwa kuwathamini na kuwapa elimu watoto wa kike ili kupunguza unyanyasaji wa kijinsia unaoendelea kwa sasa.
Kwa upande wake mkurugenzi kituo cha matumaini centre HELLEN NKUNDA amesema kuwa amekuwa akipokea watoto wengi wa kike ambao wamefanyiwa ukatili wa kijinsia na amekuwa akiwapokea na kuwapa elimu ya ufundi.
Lakini NKUNDA amewataka watoto hao kuwa makini na waaminifu katika maisha yao ili wasirudie yale ambayo yalimtokea hapo awali na wasikubari kudanganywa tena.
NKUNDA ameitaka serikali kutoa elimu kuanzia shule ya msingi juu madhara ya ukatili ili kujenga jamii ambayo itakuwa na elimu juu ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsi hasa kwa watoto wa kike.
Alimalizia kwa kumshukuru mwandishi wa habari frank kibiki kwa kutoa msaada wake kwa mtoto ambaye aliyekuwa amefanyiwa ukatili wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment