Thursday, 23 April 2015

KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA HASSAN MTENGA AENDELEA KUVURUNGA MIPANGO YA WAPINZANI KATIKA JIMBO LA ISMANI




katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akiwahutubia wananchi wa tarafa ya pawaga.





katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akijibu maswali ya wananchi wa tarafa ya pawaga.





katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akiwapa vifaa vya michezo wananchi wa tarafa ya pawaga






na fredy mgunda,pawaga


katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa iringa hassani mtenga amewataka wananchi wa tarafa ya pawaga katika jimbo la isimani kuendelea kumwamini mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa anawatendea haki kwa kuwaletea maendeleo.


akizungumza katika mkutano huu katibu wa chama hicho MTENGA amewataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kutokana na kutekeza ahadi zao ambazo wanakuwa wanaziahidi kwa wananchi.


Kwa upande wao wananchi kijiji cha boliboli kilichopo tarafa
ya pawaga wilaya ya iringa vijijini wanakabiriwa na matatizo ya kiafya pamoja na migogoro ya aridhi baina ya wafugaji na wakulima hayo yamebaini katika mkutano ulifanyika katika kijiji
hicho.


wakizungunza wakati wa mkutano huo wananchi hao wamesema
kuwa kijiji hicho hakina mganga wa kutoa huduma katika zahanati yao na kuongeza kuwa tatizo la migogolo ya aridhi
limekuwa kubwa.


Akijibu maswali ya wananchi hao katibu wa ccm mkoa wa iringa
hassani mtenga amewata viongozi wa chama hicho kufanya mikutano ya mara kwa mara na kupokea kero za wananchi na kuzitatua mapema ili kuendelea kukijengea imani chama chao.


Viongozi wengi wamekuwa hawawajali wananchi wao ambao wamewaweka matarakani na ndio imekuwa sababu ya matatizo mengi na migogolo mikubwa katika vijijini.



Lakini MTENGA amesema swala mfureji,tatizo la mganga,walimu
kuwa walevi na mgogoro wa mbomipa anayachukua na kwenda kuyafanyia kazi na kuwaahidi kuwa matatizo yote waliomweleza yatatulika.


“Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuipigia kura katiba
inayopendekezwa ili waweze kupata katiba ya wananchi na kuwaambia wananchi wa eneo hilo kuitumia fursa ya kuijiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia kura ambalo iringa litaanza tarehe 29 mwezi huu” alisema HASSAN MTENGA.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...