semina ya mafunzo ya maandalizi ya uboreshaji wa daftari la
kudumu la wapigakura iliyohusisha mratibu wa uandishaji wa mkoa, afisa
mwandishaji, maafisa waandishaji wasaidizi na maafisa uchaguzi wa halmashauri
kwa Mkoa wa Iringa.
MKOA wa Iringa unatarajia kuandikisha jumla ya wapigakura
646,575 katika daftari la kudumu ya wapigakura kwa kutumia mfumo mpya
ujulikanao kama Biometric Voters Registration (BVR) unatarajia kuanza mwishoni
mwa mwezi huu, Nipashe imedhibitisha.
Hayo wamefahamika jana wakati wa semina ya mafunzo ya
maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura iliyohusisha
mratibu wa uandishaji wa mkoa, afisa mwandishaji, maafisa waandishaji wasaidizi
na maafisa uchaguzi wa halmashauri kwa Mkoa wa Iringa.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo/jana Katibu Tawala
Msaidizi-Serikali za mitaa ambaye pia mratibu wa uchaguzi wa mkoa wa Iringa,
Wilfred Myuyu alisema kuwa katika maoteo (projection) ya awali mkoa unatarajia
kuandikisha wapigakura wapatao 646,575 pamoja na vituo vya uandishaji 1,192.
Alikitoa mchanganuo wa uandikishaji kwa kila halmashauri alisema
kuwa Manispaa ya Iringa inatarajia kuandikisha wapigakura 79,086, Halmashauri
ya Iringa (121,452), Halmashauri ya Mufindi (252,303), Mafinga mjini (74,043)
na Kilolo (118,692).
Kwa upande wa vituo vya uandikishaji katika mabano Manispaa
ya Iringa itakuwa na vituo (192), Kilolo (257), Mufindi DC (347), Mafinga TC
(76) na Iringa DC (320).
Awali wakati akifungua semina ya mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya
ya Iringa, Angelina Mabula kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza
alitoa wito kwa maafisa hao kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na tume
ili kuweza kufanya kazi vizuri wakati wa zoezi hilo.
“Napenda kusisitiza tena kwenu kwamba mkiwa maafisa
waandishaji na maafisa wasaidizi mnatakiwa kuhakikisha kwamba watu wote
wanaostahili kuandikishwa na watakaofika kujiandisha kwenye vituo wanandikishwa
na kuhudumiwa kulingana na utaratibu uliowekwa ili majina yao yawepo katika
daftari la kudumu la wapigakura,” alisema Masenza.
Aidha, katika utaratibu wa sasa, kama ilivyokuwa katika
utaratibu wa zamani, wawakilishi wa vyama vya siasa wanataruhusiwa kuwepo
katika vituo vya kuandikisha wapigakura.
“Jambo hili ni muhimu kwani linasaidia kudhihihirisha uwazi
katika zoezi zima. Wajibu wa wawakilishi wa vyama vya siasa kama ilivyoelezwa
ni kuangalia kwamba sheria, kanuni, na taratibu zilizowekwa na tume (NEC)
zinazingatiwa katika uandikishaji,” alisema mkuu huyo.
Hata hivyo, mkuu wa mkoa huyo alitoa wito kwa viongozi wa
dini kuhamasisha waumini na watu wote hususan raia wote walio na sifa za
kujiandikisha kupiga kura ili wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuandikishwa.
Aliongeza kuwa watakaojiandikishwa ni wananchi wote waliowahi
kuandikisha hapo awali, waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea na wote ambao
kwa sababu mbalimbali hawakuwahi kuandikishwa ikiwa ni pamoja na wale
watakaotimiza umri wa miaka 18 ifikapo siku ya uchaguzi, yaani Oktoba 2015.
BVR ni kifaa cha kisasa ambacho huandikisha kwa kutumia
kompyuta na kuchukua alama za vidole, saini na upigaji picha kwa ubora wa hali
ya juu ili kuondoa uwezekano wa wapiga kura kujiandikisha zaidi ya mara moja.
No comments:
Post a Comment