Friday, 3 July 2015

CCM: TUTAKATA RUFAA KESI ZA MADAI ZILIZOTUPWA NA MAHAKAMA


Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini wanatarajia kukata rufaa kupinga kuondolewa kwa kesi nane za madai zilizotupiliwa mbali na mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya iringa, ili ziwezekusikilizwa tena baada ya Chadema kupeleka pingamizi zao mahakamani.

Chama hicho kinachowakilishwa na wakili msomi, Gaster Likatage Mdegela kiliongea na Nipashe jana kuwa wako mbioni kukata rufaa kwa zile kesi za madai zilizoondolewa mahakamani awali kwa vigezo kuwa zilikosa mashiko. 

Kwa mujibu wa Wakili wa CCM, Gaster Likatage Mdegela alisema Chama cha Mapindizi (CCM) kilifungua kesi 35 za madai za uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 13.01.2015, lakini Chadema nao walipeleka pingamizi za awali 35 mahakamani ili kesi zifutwe kwa gharama na pingamizi ya kesi nane zilikubalika katika hukumu ndogo ya awali (ruling). 

Mahakama ya Wilaya ya Iringa hivi karibuni imetoa hukumu ya kutengua matokeo ya mitaa 13 kutoka Manispaa ya Iringa ili kufanya uchaguzi wa marudio wa Serikali za Mitaa kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14 mwaka 2014.

Hukumu hiyo ilitolewa jana mbele ya mahakamu wakazi wanne ambao ni Andrew Scout, John Mpitanjia, E. Nassoro na Isaya, waliokuwa wanaendesha kesi hizo katika Mahakama ya Wazi ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Iringa.

Aidha, mitaa iliyotenguliwa matokeo yake ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14, 2014 kutokana kasoro mbalimbali ni pamoja na SabaSaba Kata ya Gangilonga, Darajani na Kondoa Kata ya Mivinjeni, Ndiuka ‘D’ Kata ya Igumbulo, Kaduma Kata ya Mkimbizi na Semtema ‘A’ Kata ya Kihesa, 

Mitaa mingine ni Nyamhanga ‘B’ Kata ya Kitwiru, Muungano ‘A’na ‘B’ Kata ya Kwakilosa, Kajificheni Kata ya Ilala, Kihodombi ‘B’ Kata Isakalilo, Dodoma Road na Mkimbizi ‘B’ Kata ya Mkimbizi.

Chama cha Mapindizi (CCM) kulifungua kesi 35 za madai za uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 13.01.2015 na kuwakilishwa na wakili msomi, Gaster Likatage Mdegela dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na chama wananchi CUF, ambapo kesi 34 zilikuwa za Chadema na kesi moja tu ndio ilikuwa ya CUF.

Aidha, katika kesi hizo mlalamikiwa namba moja alikuwa ni Chadema walioshinda uchaguzi wa serikali za mitaa na mlalamikiwa wa pili alikuwa ni msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Katika upande wa walalamikiwaji walikuwa na mawakili nane waliosimamia kesi hizo ambao ni Barnabas Nyulusi, Mariam Mbano, Leah Francis, Queen Mtove, Catherine Chalwa, Charles Lawisso, Collins Malekela na Jane Massey.

Wakili Barnabas Nyulusi, alisimamia kesi zote Chadema kama madaiwa namba moja katika kesi hizo cha uchaguzi.

Moja ya kasoro hizo zilizolalamikiwa ni kuchanganywa kwa majina ya wagombea wa uenyekiti. 

mahakimu wakazi hao walitengua matokeo ya mitaa 13 ili uchaguzi kurudiwa ndani ya siku 30 bila kulipa gharama zozote za uendeshaji wa kesi kwa pande zote mbili za mlalamikaji na mlalamikiwa na rufaa iko wazi.

Kwa mantiki hiyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimegaragazwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kesi ya msingi ya madai ambapo mahakama ilitenguliwa matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili uchaguzi urudiwe katika nafasi ya wenyeviti.



Katika hukumu hiyo ambayo ilitolewa na Mahakama ya Wilaya ya Iringa Juni 30, mwaka huu imekubaliana na hoja za walalamikaji ambao ni wagombea wa CCM washinda mitaa 13 na Chadema wao walishinda mitaa sita katika ya jumla kesi 19 zilizosikilizwa.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...