MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA JIMSON SANGA
baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa zamani tumaini
baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa zamani tumaini
na fredy mgunda,iringa
Chuo kikuu cha IRINGA ZAMANI TUMAINI kesho kinatarajiwa
kuadhimisha siku ya utalii wa kitamaduni katika chuo hicho.
Akizungumza na blog hii mkuu wa kitengo cha utalii cha chuo hicho MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA JIMSON SANGA amesema kuwa wameamua kuadhimisha siku hiyo ili kuwakumbusha wananchi juu ya kuuezi utamaduni wao na kuacha kuiga tamaduni za kigeni.
Aidha SANGA amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikifundisha
elimu ya utalii ndani ya chuo tu sasa imefika wakati wa kutoka na kuifikia moja kwa moja jamii ambayo haina elimu hiyo.
“Tunaona wakina mama ntilie wanauza vyakula ya kitamaduni
lakini hawana wateja kwa sababu wanashindwa kutoa huduma ya kuridhisha kwa wateja hata hivyo mama ntilie wengine hutoa huduma kwa kutofata mazingira yakiafya”.alisema SANGA
Ameongeza kuwa watanzania wengi hatuna tabia ya kuupenda utamaduni wetu au kuipenda asili yetu tunaona wananchi wengi wanapenda kuiga utamaduni wa kigeni hivyo tunatakiwa kuuenzi utamaduni wetu.
SANGA amemalizia kwa kuwataka wanachi wajitokeze siku ya
jumamosi ili kujionea vitu mbalimbali ya kitamaduni.
Kwa upande wao WANAFUNZI WA CHUO HICHO hasa wanaosomea masomo ya maliasili na utalii wamewataka wananchi wa mkoa wa iringa kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hao.
No comments:
Post a Comment