Monday, 6 July 2015

SHAMRASHAMRA ZA MANUNUZI YA BIDHAA KATIKA BANDA LA MeTL GROUP MAONYESHO YA SABASABA


Ofisa Mtendaji wa Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack, akisikiliza maoni kutoka kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Kampuni ya MO Assurance lililopo ndani ya banda la MeTL Group katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.


Meneja mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO, (MO ASSURANCE), Ravinshankar Venkatrama (kulia) akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group, Hussein Dewji alipotembelea banda la MO Assurance kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kutimu vumbi jijini Dar.


Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group, Hussein Dewji, akipata maelezo kutoka kwa kijana anayetoa huduma kwenye bidhaa za Sundries zinazotengenezwa na kampuni ya MeTL Group. Kulia ni msimamizi wa duka la bidhaa za Sundries, Sandeep Gaur alipotembelea maonyesho ya Sabasaba.


Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group, Hussein Dewji, akisalimiana Meneja wa LG tawi la Nkurumah, Bw. Yasin Lodhi (wa pili kulia) alipowasili kwenye banda la bidhaa za LG ambapo kampuni ya Mohammed Enterprises Limited Tanzania (MeTL) ndio msambazaji rasmi wa bidhaa hizo nchini.


Mfanyakazi wa kampuni ya 21st Century Textiles Ltd, Hidaya Kapera akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotembelea banda hilo linalouza vitenge vya aina mbali mbali kutoka kampuni za Afritex Ltd, Musoma Textiles Ltd na Novatexmoque ambazo zote ziko chini ya MeTL GROUP.






Mfanyakazi wa kampuni ya 21st Century Textiles Ltd, Regina Waitara, akielezea ubora wa vitenge na mashuka yanayozalishwa na kampuni hiyo kwa mmoja wa wateja aliyetembelea banda hilo.


Balozi wa bidhaa za LG, Albert Laurent akitoa maelezo ya bidhaa za LG ambazo zipo katika punguzo la bei la 15% katika msimu huu wa maonyesho ya Sabasaba na mwezi mzima wa Ramadhan kwa wateja waliotembelea banda hilo ndani ya viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere.


Wananchi wakijipatia huduma ya vinywaji baridi vya MO vikiwemo MO Cola, MO Portello, MO Embe, MO Chungwa sambamba na kinywaji cha MO BOMBA kinachokuburudisha na kukupa nguvu wakati wote.


Wateja wakiwa wamefurika kujipatia bidhaa za sabuni katika banda la bidhaa za kampuni ya Royal Soap & Detergent Industries Limited lililopo ndani ya banda la MeTL Group.


Mfanyakazi wa kampuni ya Royal Soap & Detergent Industries Limited, Saumu Hamza, akionyesha bidhaa tofauti za sabuni za unga zinazopatikana katika banda hilo.


Wateja wakifurahia sabuni za wa kampuni ya Royal Soap & Detergent Industries Limited.


Wafanyakazi wa kampuni ya Sundries chini ya MeTL Group, Shomu Bhergava (kushoto) na Sandeep Gaur (kulia) wakitoa maelezo kwa mteja alitembelea banda lao katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere, barabara Kilwa, jijini Dar es Salaam.


Balozi wa bidhaa za LG, Balbina Gabriel akimwonyesha mteja bidhaa ya Microwave ya kampuni ya LG aliyetembelea katika banda la MeTL Group kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.







Mdhibiti ubora idara ya sabuni za kampuni ya MeTL GROUP, Cuthbert Sangiwa Msuya akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi juu ya ubora wa mafuta ya kulainisha ngozi (Lotion) inayoyazilishwa na kampuni hiyo.



Wafanyakazi wa duka la vifaa vya LG lililopo ndani ya banda la MeTL Group katika picha ya pamoja na Msimamizi wa banda hilo Sakina Alloo (aliyepiga magoti).

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...