Monday, 6 July 2015

IPC WAPATA VIONGOZI WAPYA KWA MIAKA MITATU IJAYO


Msimamizi wa uchaguzi  Hakimu Mwafongo (kushoto) akitangaza matokeo katika mkutano mkuu wa tatu wa mwaka uliyofanyika Ukumbi wa Lutheran Center mjini Iringa. Kulia ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi, Sofia Mpunga.

Mgombea Tukuswiga Mwaisumbe katika nafasi ya katibu akiomba kura

Mtia nia Conrad Mpila katika nafasi ya makamu mwenyekiti akiomba kura.

Mtia nia Frederick Siwale katika nafasi ya makamu mwenyekiti akiomba kura.




Mtia nia Jackson Manga katika nafasi ya makamu mwenyekiti akiomba kura.


Mtia nia Francis Godwin katika nafasi ya katibu na makamu mwenyekiti akiomba kura.



Na Friday Simbaya, Iringa

KLABU ya Waandishi wa Habari mkoani Iringa (IPC) imepata viongozi wapya watakaokuwa madarakani kwa miaka mitatu ijayo katika uchaguzi wa mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika jana mjini Iringa.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi hayo msimamizi wa uchuguzi, Hakimu Mwafongo, akisaidiana na msaidizi wake, Sofia Mpunga alimtangaza Frank Leonard kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho kwa mara ya pili tangu aliyekuwa mwenyekiti, Daudi Mwangosi kuuawa Septemba 2, 2012 baada ya kupigwa bomu kwenye mkutano wa Chadema huko Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Alisema chama hicho kilifanya uchaguzi katika nafasi za makamu mwenyekiti na katibu mtendaji wakati nafasi za ujumbe na mwenyekiti walipita bila kupingwa.

Mchuano mkubwa ulikuwa katika nafasi ya makamu mwenyekiti ambapo wagombea walijitokeza wanne akiwemo Conrad Mpila, Frederick Siwale, Jackson Manga na Francis Godwin.

Hata hivyo, Fredrick Siwale aliibuka mshindi katika nafasi ya makamu mwenyekiti baada ya kuwashinda wagombea wengine watatu walioomba nafasi hiyo kwa kupata kura 16.

waliogombea wengine katika nafasi hiyo na matokeo yao katika mabano ni Conrad Mpira (1), Jackson Manga (1) na Francis Godwin (5), ambapo jumla ya wajumbe waliopiga kura ni 23.

Katika nafasi ya katibu, Tukuswiga Mwaisumbe alichaguliwa kuwa katibu mtendaji kwa kupata kura 14 baada ya kumshinda mpinzani wake Francis Godwin aliyekuwa akitetea nafasi yake kwa kupata kura (10).

Katika uchaguzi huo pia wajumbe saba waliochaguliwa ambao ni Selina Ilunga, Gertrude Madembwe, Happy Matanji, Jackson Manga, Francis Godwin, Shaban Lupimo na Frola Kamage.

Viongozi wengine waliochaguliwa bila kupingwa ni pamoja na Janeth Matondo mweka hazina na Selemani Boki mweka hazina msaidizi.

Klabu hiyo ya waandishi wa habari ina jumla ya wanachama 41, kati yao ni wanachama 31 waliohai ambao wamelipa ada na ndio walioalikwa katika mkutano mkuu huo.

Chama hicho katika kipindi cha mwaka 2013 hadi 2015 kilikusanya michango na misaada ya zaidi ya shilingi milioni 10.



Fedha hizo ni makusanyo ya akiba yanayotokana na fedha kutoka umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC), ada za wanachama na wadau wengine.





No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...