Monday, 6 July 2015

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA WAMPONGEZA KATIBU WA CCM IRINGA MJINI





katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA
MWAMPASHI






katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA
MWAMPASHI 


KEKI ILIYOKUWA IMEANDALIWA SIKU YA SHEREHE HIYO.



Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi tawi la chuo kikuu cha iringa zamani tumaini.


NA FREDY MGUNDA, IRINGA


Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi tawi la chuo kikuu cha iringa zamani tumaini wamefanya mahafari yao katika ukumbi wa chama hicho sabasaba.

Wakizungumza wakati wa sherehe hiyo wanafunzi hao wamesema
kuwa sas ccm italajia kurudisha jimbo la iringa mjini kwasababu tayari makatibu wa chama hicho wameweza kuwarudisha vijana kukipenda chama hicho.

Aidha wamesema kuwa chama hicho kilipoteza mvuto kwa vijana na vijana walipoteza mvuto na chama hicho,hivyo chama hicho kwa sasa kimerudisha imani kwa vijana na wanachama wengine.

“Sisi hapa chuoni kwetu tulikuwa wanachama wachache ila kwa sasa tupo wengi na kila siku wanachama wanazidi kuongezeka kutokana na kukipenda cha hicho kwa wakati huu tukielekea katika uchaguzi mkuu”walisema wanafunzi hao.

Mbunge wa jimbo hili kwa sasa mchungaji PETTER MSIGWA
ajiandae kuondoka kutoka na chama hicho kujipanga kila kona na tayari wamejihakikishia ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuongeza kuwa wananchi wa manispaa ya iringa wanapenda amani na sio vurugu.

Lakini walimpongeza katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA
MWAMPASHI kwa kufanya kazi nzuri iliyosababisha wananchi wa jimbo hili kurudisha imani na chama hichi na kuongeza kuwa MWAMPASHI ni kiongozi mzuri na anajua majukumu yake hivyo ni vizuri wananchi wa manispaa tukashikiana na jembe hili kulikomboa jimbo hili.

Kwa upande wake KATIBU WA JIMBO HILI ELISHA MWAMPASHE ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo aliwapongeza wanachama wa chama hicho tawi la tumaini kwa kukikuza chama hicho na kuongeza wanachama.

MWAMPASHI akawataka wanachama hao kukipigania chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao ili waweze kushinda kwa kishindo kikubwa na kuwaachawapinzani hoi.

“Tunanguvu na nia ya kufanya vizuri katika uchaguzi wa mwaka
huu kwa kuwa tumejipanga kili kona na tumerudisha inmani kwa wananchi wote hivyo kazi kwa sasa imekuwa rahisi hasa kulikomboa jimbo la iringa mjini ambalo walilikopesha kwa mpinzani”alisema MWAMPASHI.

Aidha MWAMPASHI aliwataka wananfunzi kuacha kufanya mambo ya kizinaa pindi wapatapo kazi kwa kudai kuwa anakura ujana ,akaongeza kuwa sasa ni wakati wa vijana kuwekeza katika biashara mbalimbali ili kujitengenezea maisha mazuri hapo baadae.

“Nawaomba jamani tusiwe na tamaa katika kutafuta maendeleo
kwa kuiba au kutoa na kupokea rushwa kwa kuwa hiyo njia sia sahihi kwani hapo mtakuwa mkirudisha maendeleo nyuma na sio
kuendelea kuleta maendeleo”.alisema MWAMPASHI.

Alimalizia kwa kumtaka mbuge wa jimbo hili kufungasha vitu vyake kwa kuwa muda wake umeisha na wananchi wa manispaa ya iringa wamemchoka kwa kuwa toka ameingia madarakani hakuna alichokifanya katka kuleta maendeleo ya jimbo hili zaidi kuanzisha migomo na vurugu katika sehemu mbalimbali.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...