Kushoto
kwenda kulia ni Afisa Utalii Nyanda za Juu Kusini Gervas Mwashimaha, Ofisa
Utalii wa Tanapa wa ofisi ya Utalii Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Risala
Kabongo, Kaimu Meneja Masoko TANAPA Victor Ketansi na Afisa Mawasiliano
Mwandamizi TANAPA Catherine Mbena wakiongea na wanahabari mkoani Iringa jana. (Picha
na Friday Simbaya)
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia hifadhi zake 16 linakusudia kukusanya zaidi ya 2.5bn/- katika kampeni ya kuhamasisha watu kutembelea hifadhi za taifa ili kuhamasisha utalii wa ndani, yeney kauli mbiu yake, “Tembelea Hifadhi Uzawadike.”
Kaimu Meneja Masoko TANAPA, Victor Ketansi akiongea na waandishi mkoani Iringa jana iliweka msisitizo katika kutangaza na kuhamasisha utalii wa ndani ili kupunguza utegemezi kwa watalii wa kigeni.
Alisema kuwa TANAPA kwa kushirikiana na makala wa utalii (tour operators)katika kampeni hiyo ya miezi sita (6) iliyoanza Julai 1 hadi Desemba 31, 2015 watanzania watumia fursa hii kutembelea Hifadhi za Taifa na kujipatie zawadi kemkem katika kipindi hiki cha kampeni.
Alisema kwa pamoja na kwamba utaburudika, kushangaa na kufurahia kuona vivutio mbalimbali, pia utapata zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa kila atakayetembelea hifadhi wakati huu wa uhamasishaji.
“Washirika/wadau wetu wapo katika mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Iringa, Morogoro na Mbeya mjini,” alisema kaimu meneja masoko wa TANAPA.
Zawadi zitakazotolewa ni DVD za wanyama,Vitabu vya wanyama, Tshirts, Kofia, Tai za TANAPA, zawadi nono ya kwenda kutalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti au Gombe kwa muda wa siku TATU na kulala katika hotel yenye hadhi ya Nyota tano.
Hata hivyo, Kaimu Meneja Masoko TANAPA, Victor Ketansi alisema kuwa tangu kuanzisha kwa kampeni za kuhamasisha jamii tembelea hifadhi za taifa utalii wa ndani umeomgezeka ambapo kwa mwaka watalii 427,208 alitembea hifadhi za taifa.
Kwa Hifadhi ya Saanane na Kilimanjaro zawadi itatolewa kwa taasisi itakayopeleka idadi kubwa ya watalii.
Kampeni hii na zawadi husika haziwahusu wafanyakazi katika kampuni za kitalii na mahoteli yaliyoko ndani na hifadhi.
Mchanganuo wa Zawadi zitakazotolewa.
Katika kipindi hiki cha kampeni kwa yeyote atakayetembelea hifadhi zaidi ya mara moja atapata zawadi isipokuwa kwa hifadhi za Taifa Saanane na Kilimanjaro (Hizi zina zawadi kwa utaratibu tofauti).
Ukitembelea hifadhi ya Taifa yoyote zaidi ya mara moja utajipatia DVD yenye wanyama mbalimbali.
Ukitembelea hifadhi ya Taifa yoyote zaidi ya mara mbili utapata DVD ya wanyama na fulana ya TANAPA, Kofia au Tai.
Ukitembelea hifadhi ya Taifa yoyote zaidi ya mara tatu utajipatia DVD yenye wanyama mbalimbali, fulana, Kofia, Tai na Kitabu cha wanyama.
Ukitembelea hifadhi zaidi ya mara nne utapata zawadi zote hapo juu pamoja na zawadi ya juu kabisa ambapo, utapelekwa kutalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti au Gombe (kuangalia sokwe) na kulala katika hotel yenye hadhi ya nyota tano kwa muda wa siku TATU kwa gharama za TANAPA.
Kwa hifadhi za Kilimanjaro na Saanane: Itazawadiwa taasisi au mtu itakayo peleka wageni wengi zaidi kipindi cha kampeni hii Julai- Disemba, 2015.
Saanane-Mtu atakayepeleka watalii wasiopungua 1500 atapewa zawadi ya juu kabisa
Kilimanjaro -Taasisi itakayopeleka watalii wasiopungua 150 kwa kipindi chote cha kampeni itajipatia zawadi ya juu kabisa.
MUDA WA KAMPENI
Kampeni hii itakuwa ya miezi sita (6). Kuanzia Julai 1 hadi Disemba 31, 2015
VITUO VYA KUJIANDIKISHA NA KULIPIA
Vituo vipo mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Iringa, Morogoro na Mbeya Wadau wa utalii wote (tour operators) wanakaribishwa kushiriki.
Muhimu kwa watalii wetu:
Kujiandikisha jina na namba ya kitambulisho cha aina moja kila aingiapo hifadhini ili tumtambue kwa ajili ya zawadi.
Wenye usafiri binafsi wanaweza tembelea hifadhi bila kupitia vituo vilivyotajwa hapo juu.Wazingatie kujiandikisha katika kitabu maalum kilichopo katika lango la kuingilia hifadhini.
Huduma za malazi ya bei nafuu ndani ya hifadhi zinapatikana. Vituo vyetu vilivyotajwa hapo juu vitatoa taarifa zote kwa aina ya utalii wowote unaohitaji ndani ya hifadhi.
Sheria na taratibu za hifadhi ziendelee kuzingatiwa wa kutoa elimu ya uhifadhi ili kuhakikisha jamii inanufaika na shughuli za uhifadhi katika maeneo yanayozunguka hifadhi.
No comments:
Post a Comment