na mwandishi wetu jimmy kagaruki,dar
Mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) DKT FENELA MUKANGARA amesema atashirikiana na wananchi wa jimbo la kibamba kupambana na kero ya maji kwenye jimbo hilo.
Akizungumza na nuru fm MUKANGARA amesema licha ya mikakati ya serikali ya kupambana na kero ya maji kwa wakazi wa jiji la dar-es-salaam na jimbo la kibamba kwa ujumla bado kuna upungufu wa maji kwa wakazi hao.
Ametaja sababu za upungufu huo wa maji kuwa ni pamoja na baadhi ya wananchi wasio waaminifu kujiunganishia mitandao ya maji kiholela kwa ajili ya biashara na uchakavu wa mabomba kutoka mtambo mkubwa wa maji wa ruvu juu.
MUKANGARA ameongeza kusema kuwa suala la wananchi wote kufikishiwa maji majumbani litachukua muda na hivyo kusisitiza nguvu ya pamoja itumike kutoka serikalini na wadau wa sekta ya maji na wafadhili kushirikiana kuchimba visima virefu na vifupi ili kukabiliana na kero hiyo.
Aidha kutokana na umuhimu wa maji, MUKANGARA ametoa rai kwa wananchi wa jimbo la kibamba kutoa taarifa kwenye mamlaka husika dhidi ya wale wote wanaohujumu miundo mbinu ya maji ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
No comments:
Post a Comment