MGOMBEA wa Ubunge kupitia jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Jospeh Mbilinyi “Sugu” ni kama ameshajihakikishia ushindi ndivyo unaweza kusema baada ya mikutano yake yato ya kampeni kupata mwitikio mkubwa wa watu.
Sugu ambaye anaungwa mkono pia na vyama vinavyounda Ukawa ambavyo ni CUF,NCCR-Mageuzi pamoja NLD, ambapo leo akiwatubia wakazi wa Igawilo-Uyole mjini Mbeya, mkoani hapo, huku akisimamisha shughuli za kijamii katika maeneo hayo baada ya wakazi wengi kujitokeza kama unavyoona pichani.
Ambapo Sugu amewataka wakazi wa Mbeya kutofanya makosa makubwa tena kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi CCM kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kwa kusema hakina nia ya dhati ya kumkomboa mtanzania ikiwemo mkoa wa mbeya ambao amedai licha ya kuwa na mali nyingi anasikitika kwanini wananchi bado ni masikini.
No comments:
Post a Comment